Thursday, 12 May 2022

WANAWAKE KAGUNGA WALIA KUTELEKEZWA

...
 
Wananchi wa vijiji vya Kagunga na Zashe wilaya ya Kigoma mkoani wakisikiliza maelezo kuhusu utoaji wa taarifa kwenye vituo vya taarifa na maarifa kusaidia kutoa taarifa za vutendo vya ukatili vinavyotokea kwenye maeneo yao.
**

Na Fadhili Abdallah,kigoma

 

Wanawake wanaoishi katika Kata ya Kagunga wilaya ya Kigoma Mkoani Kigoma Mpakani mwa Tanzania na Burundi wamelalamikia vitendo vya waume zao kutelekeza familia na hivyo kusababisha maisha duni ya wanawake na watoto.

 

Wakizungumza wakati watendaji wa Mtandao wa jinsia Tanzania (TGNP) wakiendesha mkutano ya uelimishaji na uhamasishaji jamii kutoa taarifa kwa mamlaka za serikali na wadau wa kuzuia ukatili ikiwa ni mpango wa mtandao huo kuiongeza uelewa kwa jamii kupiga vitendo vya ukatili kwa wanawake na watoto.

 

Mmoja wa wanawake hao,Lucia Marco alisema kuwa kutokana na kutelekezwa huko familia nyingi zimekuwa zikiendeshwa na wanawake ambao wengi wao hawakuwa na shughuli za kiuchumi hivyo kusababisha hali ngumu kwa familia kupata mahitaji ya msingi sambamba na kuchangia wanafunzi kuacha kwenda shule kwa kukosa mahitaji muhimu ya shule.

 

“Familia nyingi zimebaki zikilelewa na wanawake ambao kulingana na Jiografia ya eneo hilo imekuwa ni vigumu kuendesha maisha kwani Shughuli kubwa ya kiuchumi inayofanyika ni Uvuvi ambao kwa akina mama imekuwa ni vigumu kujishughulisha nayo,”Alisema Licia Marco.

 

Naye Sabina Marco alisema kuwa miongoni mwa sababu zinazochangia wanaume kutekeleza familia kunatokana na wivu wa kimapenzi ambapo mwanaume anakuwa na wanawake wengine wan je hivyo migogoro ya kifamilia inapoanza wanaume huondoka na kuhamia kwa wanawake hao hasa wale wenye uchumi na wanajishughulisha na shughuli zinazowaingizia kipato.

 

waume zmmoja wa wananAidha wameeleza Ujirani na nchi ya Uburundi nao umekuwa ukichochea Familia nyingi kutengena hasa kwa wakazi wa vijiji jirani kutoka nchini humo wanapoingia katika eneo hilo na kuanzisha uhusiano na na wanaume au wanawake ambal tayari wanakuwa na familia.

 

Aidha inaelezwa kuwa baadhi ya wavuvi kutoka Burundi wanapofika maeneo yao kwa shughuli za uvuvi wanajenga mahusiano na kuwazalisha na baadaye kurudi kwao wakiwaacha wanawake na watoto bila msaada wowote.

 

Akieleza kuhusu uwepo wa changamoto hiyo Afisa maendeleo ya Jamii halmashauri ya wilaya ya Kigoma, George Mselem alisema kuwa katika  Kukabiliana na changamoto hiyo wameanza kutoa elimu kwa wanawake kutoka makundi mbalimbali wakiwemo wajane na waliotelekezwa kujiunga kwenye  Vikundi vya uzalishaji  ili iwe rahisi kupata mikopo na kuanzisha shughuli za kuwaingizia kipato.

 

Alisema kuwa pamoja na hilo wamekuwa wakitoa elimu na kuhamasisha wakina mama hao kutoa taarifa za vitendo vya ukatili na utelekezwaji wa familia ili waweze kufuatilia waume zao waweze kuhudumia familia hata kama hawapo nyumbani ambalo ndiyo jukumu lao la Msingi.

 

Akizungumza katika mikutano hiyo Mratibu wa vituo vya taarifa na maarifa vinavyosimamiwa na Mtandao wa jinsia Tanzania (TGNP), Flora Ndabaniye  alisema kuwa nia ya kuendesha vituo hivyo ni kuwezesha kutolewa kwa taarifa za vitendo vya ukatili wa kijinsia vinavyofanywa kwenye ngazi ya familia.

 

Alisema kuwa vituo hivyo vinawezesha kutolewa kwa elimu kwa jamii ili waone na kujua umuhimu kwa wahanga wa vitendo vya ukatili kutoa taarifa ili watuhumiwa wa vitendo hivyo waweze kuchukuliwa hatua.

 

Kata ya Kagunga inaundwa na Vijiji 13 ambavyo kwa ujumla ni wakazi 2406 ambao kwa zaidi ya asilimia 90 wanategemea uchumi wa Ziwa Tanganyika kupitia shughuli ya Uvuvi.

Amina Joseph mkazi wa Kagunga akizungumza kwenye kikao hicho kuhusu masuala ya ukatili
Ashura Yassini akizungumza kwenye kikao hicho kuhusu masuala ya ukatili

 

Wananchi wa vijiji vya Kagunga na Zashe wilaya ya Kigoma mkoani wakisikiliza maelezo kuhusu utoaji wa taarifa kwenye vituo vya taarifa na maarifa kusaidia kutoa taarifa za vutendo vya ukatili vinavyotokea kwenye maeneo yao.


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger