Kaimu Kamanda Jeshi la Polisi mkoani Mtwara, ACP Nicodemus Katembo
Jeshi la polisi Mkoani Mtwara, linawashikilia watu wawili na mmoja bado anatafutwa na jeshi hilo kwa tuhuma za kumbaka kisha kumuua Elizabet Steven Peter (41) mkazi wa Kijiji cha Mkajamila wilaya ya Masasi Mkoani humo.
Akizungumza na waandishi wa Habari Mkoani hapo, Kaimu Kamanda Jeshi la Polisi mkoani humo, ACP Nicodemus Katembo amesema, tukio hilo linadaiwa kufanyika, Mei 6 mwaka huu, ambapo inadaiwa watuhumiwa hao walimbaka marehemu na kisha kumvunja shingo kwa kile kinachodaiwa kuwa ni wivu wa mapenzi.
Aidha katika tukio lingine Polisi mkoani Mtwara wanafanya uchunguzi wa kifo cha Hassan Mumwela, (35) mfanyabiashara na mkazi wa Kijiji cha Namhi Kata ya Libobe Wilaya ya Mtwara, baada ya mfanyabiashara huyo, kuanguka ghafla na kupoteza maisha akiwa katika eneo lake la biashara.
Chanzo- EATV
0 comments:
Post a Comment