Wednesday, 11 May 2022

UKOSEFU WA UMEME, MIUNDO MBINU DUNI KIKWAZO KWA UWEKEZAJI NA BIASHARA KIGOMA

...

Washiriki wa kongamano la biashara na uwekezaji kutoka nchi tano zinazozunguka ziwa Tanganyika na nchi za maziwa makuu wakifuatilia mwenendo wa mada zinazowasilishwa kwenye kongamano hilo. (Picha na Fadhili Abdallah)
Washiriki wa kongamano la biashara na uwekezaji kutoka nchi tano zinazozunguka ziwa Tanganyika na nchi za maziwa makuu wakifuatilia mwenendo wa mada zinazowasilishwa kwenye kongamano hilo.
Washiriki wa kongamano la biashara na uwekezaji kutoka nchi tano zinazozunguka ziwa Tanganyika na nchi za maziwa makuu wakifuatilia mwenendo wa mada zinazowasilishwa kwenye kongamano hilo.
Washiriki wa kongamano la biashara na uwekezaji kutoka nchi tano zinazozunguka ziwa Tanganyika na nchi za maziwa makuu wakifuatilia mwenendo wa mada zinazowasilishwa kwenye kongamano hilo.



Na Fadhili Abdallah,Kigoma

CHAMA cha Wafanyabiashara wenye viwanda na kilimo (TCCIA) kimesema kuwa kuondolewa kwa changamoto ya miundo mbinu ya usafirishaji kwa njia ya barabara na meli kutawezesha biashara baina ya mkoa Kigoma nan chi za maziwa makuu kuwa na tija kubwa.

Mwenyekiti wa TCCIA mkoa Kigoma,Abdul Mwillima akizungumza katika kongamano la biashara la nchi zinazozunguka ziwa Tanganyika na ukanda wa maziwa makuu ambapo amesema kuwa ukosefu wa meli za uhakika na barabara kutokuwa za viwango vya lami inakwamisha biashara na uwekezaji kufanyika vizuri.

Mwillima alisema kuwa ukosefu wa umeme wa kutosha ni kikwazo kingine ambacho kinasababisha wafanyabiashara na wawekezaji wenye nia ya kujenga viwanda mkoani Kigoma kushindwa kufanya hivyo pamoja na kuwepo kwa fursa kubwa ya biashara na uwezekaji mkoani humo.

Pamoja na hilo alisema kuwa kongamano linalofanyika litatoa changamoto nyingi ambazo zitajadiliwa na kuzitafutia njia za kuzitatua na kwamba mkoa Kigoma utafaidika kiasi kikubwa na kongamano hilo ambao kwa sasa umekuwa kama kitovu cha biashara kwa nchi za Afrika Mashairiki na ukanda wa maziwa makuu.

Akifungua kongamano hilo MKUU wa mkoa Kigoma Thobias Andengenye amesema kuwa kongamano la biashara baina ya nchi zinazozunguka ziwa Tanganyika na ukanda wa maziwa makuu ni fursa kubwa kwa nchi hizo katika kukuza uchumi ili kufikia uchumi wa kati.

Alisema kuwa kongamano hilo linaongeza msukumo ya malengo ya serikali ya awamu ya sita kuhusu kujenga uchumi wa viwanda kwa kutumia rasilimali za ndani ili kufikia uchumi wa kati mwaka 2025.

Kuwepo mpakani kwa mkoa Kigoma kunatoa fursa kubwa kuhakikisha mpango huo unatekelezeka kwa mafanikio na serikali inaendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji na biashara na kupunguza gharama za uwekezaji na biashara.

Mkuu huyo wa mkoa alisema kuwa Serikali inaendelea kutatua kero za uwekezaji nchini kupitia TIC na inaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali wakiwemo sekta binafsi ambao ndiyo wadau wakubwa kwenye kutoa ajira na uwekezaji na biashara.

Akizungumza katika mkutano huo Katibu Mkuu wa Chama cha CNDD-FDD cha nchini Burundi, Reverien Ndikuriyo alisema kuwa serikali ya Burundi imetenga kiasi cha shilingi Bilioni 200 kwa ajili ya ujenzi wa reli iendayo kasi kwenda Gitega nchini humo lengo likiwa kurahisisha usafirishaji na biashara kuelekea bandari ya Dar es Salaam.

Ndikuriyo alisema kuwa kwao Burundi Kongamano hili ni muhimu sana katika kuona namna gani wafanyabiashara na wawekezaji wa Tanzania, Burundi nan chi nyingine za Afrika Mashairiki zinashirikiana katika biashara na uwekezaji huku akieleza umuhimu wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo kujiunga na Jumuia ya Afrika Mashariki na namna itakavyowezesha kuondoa changamoto mbalimbali zilizokuwepo awali kwa nchi nyingine kufanya biashara na nchi hiyo.

Akitoa salam kwa niaba ya Mabalozi wa Tanzania kutoka nchi zinazoshiriki nchi hizo, Balozi wa Tanzania nchini Zambia, Yahaya Simba alisema kuwa hatua ya mkoa Kigoma kuandaa kongamano hili inatoa fursa chanya kwa balozi mbalimbali kutekeleza diplomasia ya uchumi kwa mafanikio na kuahidi kuunga mkono jitihada hizi zinazofanyia ili ziweze kuleta matokeo chanya.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger