Friday, 4 July 2014

STORI KAMILI: KUHUSU SHEKH ALIJERURIWA NA BOMU ARUSHA MDA WA KULA DAKU

...
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Kuhusu shekh wa Arusha aliyejeruhiwa wakati anakula Daku.
                                   

Kutoka Arusha taarifa ambayo imetangazwa kupitia Leo tena ambayo imetolewa kama breaking news ni kuhusu Sheikh wa msikiti wa Qiblatan Sood Ally Sood (37) uliopo eneo la Kilombero
jijini Arusha kulipuliwa na bomu la kurushwa kwa mkono nyumbani kwake wakati akila daku na kujeruhiwa vibaya.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo imedaiwa kuwa Sheikh huyo amejeruhiwa sehemu mbalimbali ikiwemo miguu yake yote miwili sehemu za mapajani pamoja na Kifuani na kupoteza baadhi ya vidole vya miguu yote miwili.

Mbali na Sheikh huyo pia kuna mtu mwingine aliyekuwa nyumbani kwake aliyetajwa kwa jina la Muhaji Kifea (38) ambaye ni mkazi wa Dar es salaam naye amejeruhiwa na wote wamelazwa katika hospital ya mkoa Mount Meru kwa ajili ya matibabu.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger