arusha.
JESHI la
polisi mkoani hapa limewaua majambazi watatu waliokuwa
wamepanga njama ya kwenda kupora mamilioni ya fedha zilizokuwa
zinapelekwa benki na kampuni ya Arusha Islamic Centre inayohusika na utengenezaji na uuzaji wa vigae iliyopo eneo la Esso mjini hapa.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, Kamanda wa polisi mkoani hapa, Liberatus Sabas alisema kuwa,majambazi hao watatu waliuawa jana tarehe 3 eneo la TBL -Njiro wakiwa kwenye harakati za kwenda kupora fedha hizo.
Alisema kuwa, majambazi hao walikuwa mahali wanapanga njama majira ya saa 4;20 asubuhi wakisubiria kuteka gari lililokuwa limebeba fedha zilizokuwa zinapelekwa benki zaidi ya milioni 100 huku wakiwa na gari aina ya Toyota Corola yenye namba za usajili T 762 CWE.
Alisema kuwa, raia wema walitoa taarifa kuhusiana na tukio hilo ndipo polisi walifika eneo ambalo majambazi hao walikuwa wamejificha katika eneo la unga ltd relini ambapo majambazi hao walishtuka na kuanza kuirishia gari hiyo ya polisi risasi.
Ambapo majibizano yalianza kati ya majambazi hao na polisi huku wakirushiana risasi hadi eneo la TBL njiro ndipo majambazi walipofika eneo hilo waliamua kutelekeza gari na kushuka chini na kumimina risasi kwa askari polisi hao.
Kamanda Sabas alisema kuwa,hatimaye polisi waliweza kuwauawa majambazi hao na kufanikiwa kuchukua silaha yao aina ya shortgun yenye namba A 947514 M aina ya Pumpaction ikiwa na risasi 3 .
Kamanda alisema kuwa, bado majina ya majambazi hayo hayajafahamika ambapo wanakadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 25 hadi 30 na miili yao imehifadhiwa katika hospitali ya mkoa ya mount Meru.
Aidha Kamanda aliwashukuru wananchi kwa juhudi kubwa sana walizoonyesha na ushirikiano hadi kukamatwa kwa majambazi hayo na kuwataka kuendelea kuongeza juhudi hizo zaidi.
0 comments:
Post a Comment