Friday 26 June 2015

Watu 37 wameuawa hotelini Tunisia

...
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Runinga ya taifa imepeperusha picha za shambulizi hilo
Watu wenye silaha wameshambulia hoteli moja ya kitalii iliyoko kwenye pwani ya Tunisia na kuwauwa watu 37.
Maafisa wa serikali ya Tunisia wamesema kuwa mmoja wa washambuliaji hao aliuawa kwa kupigwa risasi na maafisa wa ulinzi na kuwa waliosalia bado wanasakwa na polisi.
Shambulio hilo lilitokea katika mji wa Sousse, ambao huwavutia maelfu ya watalii kutoka bara Ulaya na Afrika ya Kaskazini.
Maafisa wa polisi wanasema kuwa mmoja wa magaidi hao ameuawa
Hili lilikuwa shambulizi la pili dhidi ya hoteli ya watalii nchini Tunisia katika kipindi cha miezi michache iliyopita.
Inaaminika kuwa washambuliaji hao waliwavamia watalii ufukweni.
Mnamo mwezi Machi mwaka huu, wanamgambo wa Kiislamu waliokuwa wamejihami kwa bunduki waliwauawa zaidi ya watu 26 katika makavazi ya Bardo, iliyoko katika mji mkuu wa nchi hiyo Tunis.
Watu 27 wameuawa hotelini Tunisia
Makavazi hayo ya Bardo hilo lilikuwa maarufu sana kwa watalii.
October mwaka wa 2013, mlipuaji wa kujitoa, alijilipua nje ya nyumba moja mjini Sousse, baada ya maafisa wa polisi kutibua jaribio lake la kutaka kuingia ndani na kuishambulia
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger