Friday 26 June 2015

Rais Kikwete aitisha kikao cha dharura cha Kamati Kuu (CCM)

...
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Rais Jakaya Kikwete ameitisha kikao cha dharura cha Kamati Kuu (CC) kitakachofanyika Kesho mjini Dodoma, huku ajenda kuu ikiwa ni kupitisha majina ya wagombea nafasi ya ujumbe wa Halmashuri Kuu (NEC), zilizo wazi kutokana na sababu mbalimbali, kuanzia ngazi za Wilaya mpaka taifa, na kwamba lazima zijazwe katika kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu ili kila mtu atimize wajibu wake.
 
Kwa mujibu wa ratiba ya Chama hicho, Kamati ya Usalama na Maadili itafanya kikao chake Julai 8 na kufuatiwa na Kamati Kuu Julai 9 ambayo inatarajiwa kuchuja wagombea wote waliotangaza nia na kupata watano ambao majina yao yatawasilishwa Halmashuri Kuu ya CCM (NEC) itakayofanyi Julai 10 kuchuja wagombea hao na kubaki watatu watakaopigiwa kura na mkutano mkuu kumpata mmoja. Mkutano huo mkuu utafanyika Julia 11 na 12.

Chanzo: MCL
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger