Serikali
imeuondoa muswaada wa sheria ya haki ya kupata habari 2015 uliokuwa
uwasilisilishwe na kujadiliwa katika mkutano unaoendelea wa bunge mjini
Dodoma ili kutoa nafasi kwa wadau kutoa maoni yao.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais (asiye na wizara maalum) Prof Mark Mwandosya
ameliambia bunge leo asubuhi kuwa serikali imefikia uamuzi huo kutokana
na maoni ya kamati ya kudumu ya bunge ya maendeleo ya jamiii iliyotaka
musawada huo uondolewe ili kutoa muda wa kujadiliwa na wadau.
Katika
taarifa yake hiyo kwa Bunge Mh. Mwandosya amewataka wadau wa habari
waendelee kutoa ushauri juu ya muswada huo pamoja na kuchangia maoni
zaidi ili kupata muswada ulio bora zaidi.
Prof
Mwandosya amesema muswada huo utawasilishwa na kujadiliwa katika
mkutano ujao wa bunge ambao utakuwa ni wa bunge la kumi na moja chini ya
serikali ya awamu ya tano.
Uamuzi
huo wa serikali umekuja kutokana na muswada huo kuzusha mgogoro na
wadau wa tasnia ya habari baada ya kuonekana kutowashirikisha wadau wa
habari moja kwa moja lakini pia kuonekana inaminya uhuru wa wananchi
kupata habari.
Wadau
mbalimbali wa habari wakiwemo chama cha wamiliki wa vyombo vya habari
MOAT wamekuwa wakilalamikia maudhui ya muswada huo kwa madai ya kuminya
uhuru wa vyombo vya habari pamoja na haki ya kupata taarifa kwa
wananchi.
Katika
mahojiano na mwanachama wa MOAT ambaye ni mwanzilishi mwenza wa mtandao
wa Jamii Forums jana (Juni 25) kupitia kipindi cha HOT MIX cha EATV
Maxence Melo, alisema kuwa endapo muswada huo ungepitishwa na kuwa
sheria, basi tasnia nzima ya habari ingekufa kwa kuwa umeweka njia ngumu
ambazo hazitekelezeki katika upatikana wa taarifa pamoja na mlolongo wa
adhabu kali kwa wadau na waandishi watakaokiuka sheria hiyo.
Naye
mwanasheria na mtafiti wa uchumi na biashara kutoka katika kituo cha
sheria na haki za binadamu Masud George kupitia kipindi hichohicho cha
HOT MIX alisema kuwa muswada huo ni hatari kwa uchumi wa nchi kwani
shughuli nyingi za kiuchumi zinategemea upatikanaji wa taarifa sahihi na
kwa wakati.
Aliongeza
pia kuwa, vyombo binafsi vya habari kama sehemu ya wawekezaji katika
sekta binafsi na chanzo muhimu cha ajira wanachangia kiasi kikubwa cha
uchumi wa nchi hivyo kuwadhoofisha ni kudhoofisha uchumi wa nchi
kiujumla.
0 comments:
Post a Comment