Read the followings story consines Godbless Lema>>>>>
MBUNGE
wa Jimbo la Arusha Mjini, Godbless Lema, amesitisha maandamano ya
kuishinikiza Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), kuongeza muda katika vituo
vya uandikishaji, kufuatia mazungumzo yake na msajili wa vyama vya
siasa nchini, Jaji Francis Mutungi.
Akizungumza
jana Arusha na waandishi wa habari, Lema, alisema juzi alipokea ushauri
kutoka kwa Jaji Mtungi asitishe maandamano na kuahidi kuja Jijini hapa
kufanya kikao na wadau wa vyama vya siasa, pamoja na waandaaji wa zoezi
hilo la uandikishaji, ili kuondoa sintofahamu inayoendelea.
Alisema
maandamano hayo waliyokuwa wayafanye Juni 25 waliyasitisha kwa barua,
baada ya Lema kuongea na Jaji Mtungi, ambaye yeye ni mdau wa jambo hilo,
kwa sababu yeye ni mlezi wa vyama vya siasa, ambaye alimuahidi atakuwa
Arusha hivi karibuni.
Lema
alisema sababu nyingine iliyowafanya waahirishe maandamano hayo ni
kauli ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Daudi Ntibenda,aliyoitoa juzi ya
kuongeza siku za kuandikishwa, katika kata za Muriet, Olsunyai,Sokoin
One, Sinoni na Moshono, ambapo ziliongezwa siku mbili.
Alisema
katika siku za nyongeza, wananchi zaidi ya 7,000 wameandikishwa, huku
wengine zaidi ya 30,000 wakiwa bado hawajajiandikisha katika kata hizo
ambazo zoezi hilo limeisha.
Zoezi
hilo Mkoani hapa lilianza katika kata sita ambazo ni Moshono, Terrat,
Muriet, Osunyai, Sokoni 1 na Sinoni ambapo kata hizo zilikuwa na jumla
ya vituo 55.
Kwa
mujibu wa Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, Juma Idd mara baada ya siku
saba kuisha zoezi hilo, litaendelea Juni 24 katika Kata ya Sekei,
Olasiti, Olomoti, Elerai, Sakina na Unga limited, ambapo kutakuwa na
jumla ya vituo 44.
Awamu
ya tatu itakuwa katika Kata ya Kimandolu, Baraa, Olorien, Themi,
Moivaro, Engutoto na Lemara ambapo kutakuwa na jumla ya vituo 55.
Awamu ya Nne ni Kata ya Levolosi, Daraja Mbili, Ngarenaro, Kaloleni, Sombetini na kata ya kati itakayokuwa na vituo 34.
0 comments:
Post a Comment