Saturday 27 June 2015

KONDA APIGA VIROBA, AZIMA!

...
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
KONDAKTA mmoja wa daladala ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja, juzikati alinaswa mchana akipiga pombe aina ya kiroba kisha kuzidiwa na ulevi hadi kufikia hatua ya kutojitambua.
Konda huyo alinaswa majira ya saa 9 alasiri maeneo ya Stendi ya Buhongwa, wilayani Nyamagana, mkoani Mwanza.
Kwa mujibu wa mmoja wa mashuhuda waliokuwepo eneo hilo,
walimuona jamaa huyo akiwa katika msongo mkubwa wa mawazo ‘stress’ haikupita muda alisogea kwenye kibanda kimoja kisha aliagiza viroba kadhaa na kuanza kunywa kimoja baada ya kingine ndipo alipozidiwa na kuangusha usingizi mzito hapohapo.
“Alikuwa hapa akisubiri daladala yake ambayo ilikuwa kwenye foleni kubwa, baadaye aliinuka na kwenda kununua viroba akaanza kunywa ndipo alipozidiwa na kuangusha ‘gari’ kabisa,” alisema shuhuda huyo.
Akiendelea kusimulia shuhuda huyo alisema;
“Baada ya zamu yake kufika, konda huyo alikuwa bado ameuchapa usingizi huku watu wakimshangaa, ndipo dereva wake alipoamua kujiongeza ‘chap chap’ kwa kuchukua konda mwingine na kuendelea kupiga mzigo,” alisema shuhuda huyo.
Mpaka shuhuda wetu anatoka eneo la tukio konda huyo alikuwa bado amelala ‘fofofo’
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger