Awali
mapema asubuhi aliomba mwongozo ripoti ya uchunguzi kuhusu ufisadi wa
bilioni 238 za ununuzi mabehewa feki iletwe lakini spika kapangua
akasema kamati ndio ina haki ya kuleta bungeni na sio mbunge.
Kwa
mujibu wa Kafulila wakati akichangia mara ya pili alisema ufisadi huu
unahusu Wizara ya Uchukuzi na Wizara ya Fedha. Hivyo Mwakyembe, katibu
mkuu, Waziri Fedha na Katibu Mkuu wa Wizra ya Fedha wote wanahusika
kwani mlipaji mkuu ni Wizara ya Fedha sasa inawezekanaje malipo
yafanyike kabla ya mabehewa kuletwa kama sio ufisadi.
Alihoji
zaidi kwanini Spika hataki serikali ilete ripoti hiyo bungeni ili mbivu
na mbichi zijulikane au kwa sababu ni kipindi cha lala salama imebaki
kila waziri anakwapua tu wizarani kwake?.
"Nasisitiza
ripoti ya wizi huu ni lazima iletwe bungeni ili bunge lijadili na
kuamua. Hamuwezi kudanganya watu kwamba mnaongeza kodi kwenye mafuta ili
mpate pesa za miradi ya umeme wakati kuna zaidi ya bilioni 238
zinapotea", alisema.
Ripoti
ya PPRA ipo wazi kwamba kampuni ya India ya Hindustan ilipewa zabuni
bila kufanya uchunguzi wa uwezo na weledi wa kampuni hii, kwamba Wizara
ya Fedha ilifanya malipo yote kabla ya mabehewa kuletwa. Na mbaya zaidi
mabehewa yaloletwa ni feki. Sasa kwanini serikali iendelee kuficha?.
Kwanini bunge nalo linajinyima meno kuchukulia hatua watu hawa?
Pia alimtaka Spika wa Bunge kuwa sehemu ya bunge na sio serikali.
0 comments:
Post a Comment