Monday 29 June 2015

BINTI AGOMA KUFUNGA ANASWA NA WANAUME 2

...
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY


2
polisi wakitekeleza majukumu yao waliushirikisha uongozi wa serikali ya mtaa huo.
Dustan Shekidele, Moro
Ni ndani ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani! Katika hali ya kushangaza, binti aliyejitambulisha kuwa ni mtoto wa Mzee Abass (20), mkazi wa jijini Tanga anadaiwa kugoma kufunga kisha kutoroka kwao na kunaswa geto na wanaume wawili mkoani hapa.
Sekeseke hilo lililofunga mtaa na kujazaa umati lilijiri Ijumaa iliyopita, majira ya saa 1:00 asubuhi kwenye Mtaa wa Mbago-Manzese Kata ya Mafiga mkoani hapa ambapo baba mdogo wa binti huyo alitoa taarifa kwa kamanda wa Oparesheni Fichua Maovu (OFM) ya Global Publishers na Jeshi la Polisi ambao waliingilia kati na kuvamia geto hilo.
5Polisi wakiwa wamemuweka binti huyo chini ya ulinzi.
Polisi walipoingia kwenye geto hilo walimkuta binti huyo na mmoja wa wanaume hao ambaye alijitambulisha kwa jina moja Rajabu.Wakati polisi wakitekeleza majukumu yao waliushirikisha uongozi wa serikali ya mtaa huo.Hata hivyo, kufumba na kufumbua mwanaume aliyekutwa na binti huyo alipata upenyo akatimua mbio na kumwachia msala binti huyo.
Mbele ya mjumbe wa serikali ya mtaa huo, Amiri Bawaziri, binti huyo alikiri kutoroka kwa wazazi wake Tanga na kwenda kuishi na jamaa huyo ambapo kwenye geto hilo pia kuna mwanaume mwingine ambaye huwa wanalala watatu kitanda kimoja.Kwa mujibu wa baba mdogo wa binti huyo, msichana huyo amemaliza kidato cha nne ambapo wazazi walikuwa wakimtafutia chuo.
4Polisi wakijiandaa kuondoka naye kwa ajili ya hatua nyingine.
Alipotakiwa kuelezea namna walivyogundua kuwepo kwenye geto hilo baba mdogo huyo alisema:
“Tulimtafuta rafiki yake ambaye baada ya kumbana alisema binti yetu yupo hapa Morogoro na amekuwa akiwasiliana naye kupita simu ya huyo mwanaume wake ambaye walifahamiana kupitia mtandao wa kijamii wa Facebook.
3….majirani na mashuhuda wakitoa maelezo au kuelezea juu ya tukio hilo.
“Baada ya kuwasiliana na namba hiyo, tulitumia mbinu za kumdanganya mwanaume huyo hadi tukapajua kwenye geto lao kweli na tumefanikiwa kumpata.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger