Habari ndugu;
Ninamatumaini
makubwa kuwa umzima wa afya na unaendelea vyema katika shughuli zako za
kila siku.natambua na kuheshimu mchango wako ikiwa ni moja ya
miongoni mwa jitihada katika kuhakikisha taifa letu linakwamuka kiuchumi
na kujiletea maendeleo kupitia nafasi yako ya kazi.
Leo
ninaomba nikushirikishe wimbo huu mpya ambao umefanywa na vijana 20
ambao wameingia katika hatua nyingine ya juu zaidi baada ya kuchujwa
kutika kundi la vijana zaidi ya 17510 waliojitokeza katika usahili wa
KINONDONI TALENT SEARCH 2015 pale Coco Beach.. hawa vijana 20 hawa ndio
pekee waliopita viwango vyote na kuonekana ni waimbaji bora ambao wako
tayari kwa ajili ya kuchujwa na hatimaye kumpata mshindi hapo baadae
mwezi ujao..wimbo unaitwa KIPAJI CHAKO AJIRA YAKO ambayo kauli mbiu hii
inabeba maana nzima ya dhima na kusudi la kuanzishwa kwa mashindano haya
ikiwa ni kuhakikisha kila mkazi wa Kinondoni ananufaika na kipaji
chake alichopewa na Mungu…nafurahi kwani nina matumaini kwa nafasi yako
uliyonayo utaifanikisha nyimbo hii kuwafikia wasikilizaji wote Tanzania
kwani hata hivyo ujumbe ulioko katika wimbo huu unawahusu vijana wote
Tanzania walioo na ndoto zao mtaani kupitia vipaji vyao.. ila wamekata
tamaa hawajui wapi waanzie.. vijana wenzao wameona wawape moyo kwa wimbo
huu maalumu..
Paul Makonda-DC Kinondoni
Jina la wimbo – KIPAJI CHAKO AJIRA YAKO
Mtunzi/composer – PETER MSECHU
Mpangilio wa mziki/music director – PETER MSECHU
Studio live recording – REAL STUDIO
Producer – MASANJA
Enjoy the music
0 comments:
Post a Comment