Magari yaliyokuwa katika msafara wa Hisham Barakat baada ya kushambuliwa kwa bomu.
Mojawapo ya gari likiwa limeharibiwa vibaya baada ya shambulio.
Dereva huyu alinusurika katika shambulio hili mbali na gari lake kuharibiwa.
KIONGOZI wa mashtaka nchini Misri, Hisham Barakat amefariki dunia
baada ya kujeruhiwa katika shambulio lililolenga msafara wake huko
Cairo, Misri.Msafara wa Bwana Barakat ulishambuliwa kwa bomu ulipokuwa ukipitia katika Wilaya ya Heliopolis leo.
Msemaji wa Wizara ya Afya Misri, Hossam Abdel Ghafa amethibitisha kifo cha Barakat kuwa kimetokea kutokana na majeraha aliyoyapata baada ya gari lake kupigwa bomu.
Barakat amekuwa akipendekeza mamia ya wapiganaji kufunguliwa mashtaka tangu kupinduliwa kwa rais aliyepinduliwa, Mohamed Morsi mwaka 2013.
Kundi linalojiita Popular Restistance of Giza limekiri kutekeleza shambulizi hilo.
0 comments:
Post a Comment