Tuesday, 22 January 2019

SULUHISHO LA UVAMIZI WA ARDHI NA HIFADHI ZA WANYAMA PORI NCHINI

...
Tanzania inapanga kutathmini upya mipaka ya hifadhi na mbuga zake za wanyama pori na misitu katika kukabiliana na ongezeko la matumizi ya radhi.

Rais John Magufuli ameagiza kusitishwa kwa mpango wa kuwatimua wakaazi wa vijiji vilivyopo kwenye hifadhi za wanyama pori na misitu.

Wizara husika zimetakiwa kutambua na kubaini hifadhi zote na misitu ambazo hazina wanyama pori zitakazoweza kugawanya kwa wakulima na wafugaji ambao wameweka makaazi katika baadhi ya hifadhi nchini.

Hatua hiyo imenuiwa kukabiliana na kuongezeka kwa matumizi ya ardhi hususan kwa jamii za wafugaji na wakulima waliojikita katika maeneo hayo ya hifadhi za wanyama pori.

Taarifa zilizopo ni kwamba wizara zote husika zinapaswa kutekeleza agizo hilo pasi kuchelewa.

Jamii tofuati kama ya Wamaasai ambao ni wafugaji, pia ni wanaohama hama katika kutafutia mifugo yao malisho ni sehemu ya watu wanaoishia kuishi katika hifadhi za wanyama pori.

Mwandishi, mkaazi mjini Arusha, Jane Edward alisema   Ngorongoro ni mojawapo ya hifadhi Tanzania ambapo binadamu wanaishi katika makaazi ya wanyama kwa muda mrefu.

Ameeleza kwamba hilo ni mojawapo ya kivutio kikubwa kinachoitambulisha hifadhi hiyo.

Chanzo:Bbc
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger