Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi, akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mgwhira vitambulisho
Wakuu wa Mikoa yote nchini wamekabidhiwa vitambulisho vya awamu ya pili vya wafanyabiashara wadogowadogo leo Jumatatu, Januari 28, 2019, Ikulu Jijini Dar es salaam.
Jumla ya vitambulisho milioni moja na laki moja vimekabidhiwa kwa wakuu hao wa mikoa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, ambavyo viliasisiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli mwishoni mwa mwaka uliopita.
Balozi Kijazi amekabidhi vitambulisho hivyo na kuwataka wakuu wa mikoa hiyo kuhakikisha vitambulisho hivyo vinatolewa kwa wahusika na kwa wakati kwa wahusika na kuongeza kuwa tayari kuna taarifa za baadhi ya watumishi wa halmashauri ambao wanaviuza vitambulisho hivyo kwa zaidi ya bei elekezi iliyotolea na Rais.
Pia amewataka wakuu hao wa mikoa kuwachukulia hatua za kinidhamu wale wote wanaokiuka agizo hilo.
Amewataka wakuu hao wa mikoa kusimamia kikamilifu zoezi hilo la ugawaji wa vitambulisho kwa wafanyabiashara wadogo wadogo huku akitaja idadi ya vitambulisho ambavyo kila mkoa utakabidhiwa.
0 comments:
Post a Comment