Sunday, 27 January 2019

KARIOBANGI SHARKS MABINGWA SPORTPESA...WAMEICHAPA BANDARI FC

...

Kariobangi Sharks

Klabu ya soka ya Kariobangi Sharks ya Kenya imefanikiwa kubeba ubingwa wa SportPesa baada ya kuifunga Bandari FC ya hukohuko nchini Kenya.

Mchezo huo uliopigwa katika Uwanja wa Taifa, Kariobangi ilipata bao lake kupitia kwa Harrison Mwendwa katika dakika ya 61 ya mchezo, ambao mpaka unamalizika, Kariobangi Sharks imeondoka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Bandari.

Hii ni mara ya tatu kwa timu za Kenya kushinda ubingwa huo, klabu ya Gor Mahia ikiwa imeshinda mara mbili mfululizo na Kariobangi ikishinda mara moja ambayo ni mwaka huu.

Bingwa wa michuano hiyo anajinyakulia kiasi cha Dola 30,000 huku mshindi wa pili ambaye ni Bandari FC akijinyakulia kiasi cha Dola 10,000, nafasi ya tatu ikenda kwa Simba ambayo inajinyakulia kiasi cha Dola 7,500.

Bingwa wa michuano hiyo, Kariobangi Sharks anapata nafasi ya kucheza na klabu ya Everton inayoshiriki Ligi Kuu ya nchini Uingereza EPL.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger