Na Theopista Nsanzugwanko - Habarileo
Serikali ya Kenya imetangaza kuongeza mishahara kwa wafanyakazi wa ndani katika miji mikubwa kufi kia Shilingi za Kenya 13,500, ambayo ni sawa na zaidi ya 300,000 za Tanzania.
Lakini, kwa upande wake, Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) limesema katika kuhakikisha mishahara inapanda katika sekta za umma na binafsi baada ya kukaa kwa zaidi ya miaka mine, wameunda tume maalum kwa ajili ya kuchambua sababu za kutaka mishahara kupanda.
Tume hiyo itaangalia namna ya kupanda mishahara kwa wafanyakazi wote, wakiwemo wa ndani, kwa kuongeza kima cha chini cha sasa cha Sh. 100,000.
Kwa Kenya, wizara inayoshughulikia masuala ya ajira imetaka waajiri katika miji mikubwa, kuwalipa wafanyakazi wa kazi za ndani kiwango hicho cha mshahara, hasa kwa wanaoishi miji mikubwa ya Nairobi, Mombasa na Kisumu.
Aidha, wale wanaoishi katika Manispaa na Halmashauri za miji watawalipa wafanyakazi wao mishahara ya Shilingi za Kenya 12,522, sawa na Shilingi za Tanzania 284,586 au Shilingi za Kenya 600 sawa na 13,600 kwa siku .
Hatua hiyo imetokana na wafanyakazi wa ndani kuandamana katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi katika Viwanja vya Uhuru Park. Wafanyakazi watakaonufaika na malipo hayo mapya ni wafanya usafi, wasimamizi wa bustani, waangalizi wa watoto, wasaidizi wa kazi za ndani, walinzi na wahudumu.
Marekebisho hayo yamesainiwa na Waziri wa Kazi, Ukur Yattani Desemba 19. Alisema agizo hilo jipya la mishahara, litaongezwa katika posho ya nyumba kwa wafanyakazi. Pia waajiri wanatakiwa kutoa michango katika mifuko ya hifadhi ya jamii kwa mwezi.
0 comments:
Post a Comment