Tuesday, 29 January 2019

MTOLEA AAPISHWA RASMI KUTUMIKIA UBUNGE TEMEKE

...
Mbunge wa Temeke (CCM), Abdallah Mtolea leo Jumanne Januari 29,2019 ameapishwa bungeni jijini Dodoma.

Mtolea ameapishwa baada kupita bila kupingwa kutokana na wagombea wa vyama vingine kukosa vigezo.

Alikuwa mbunge wa jimbo hilo kwa tiketi ya CUF na alijiuzulu Novemba 15, 2018 na kujiunga CCM.

Hata hivyo, kiapo cha Mtolea leo kilikuwa tofauti na viapo vya wabunge wengine waliohamia CCM kutokea upinzani kutokana na kutokuwa na mbwembwe zilizozoeleka.

Mtolea aliingia akisindikizwa na wabunge wachache wa CCM. Mara baada ya kuapishwa na Spika, Job Ndugai alikwenda moja kwa moja kusalimiana na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Profesa Adelardus Kilangi na Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenister Mhagama.

Wakati Mtolea akiapishwa wabunge wa upinzani waliokuwepo bungeni ni wa CUF upande wa mwenyekiti wa chama hicho, Profesa Ibrahim Lipumba.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger