Kitengo cha usalama nchini Misri, kimetoa maagizo kwamba, mashabiki wanaotakiwa kuingia uwanjani kushuhudia mchezo kati ya Al Ahly dhidi ya Simba wasizidi 10,000.
Al Ahly itacheza na Simba Jumamosi hii kwenye Uwanja wa Borg El Arab uliopo Alexandria nchini humo ambapo uwanja huo una uwezo wa kubeba watazamaji 860,000.
Agizo hilo limekuja ikiwa ni kwa ajili ya kiusalama zaidi ambapo tahadhari imechukuliwa ili kusiwe na aina yoyote ya kukosekana kwa amani.
Kama uwanja huo ungeruhusiwa kuingiza mashabiki kama ilivyo uwezo wake, ingekuwa shida kubwa kwa Simba, lakini kwa sasa inaweza kupunguza presha kwa wawakilishi hao wa Tanzania na kucheza kwa kujiamini sana.
Mchezo huo wa Kundi D katika michuano hiyo, ni wa tatu kwa timu hizo ambapo Al Ahly inaongoza kundi hilo ikiwa na pointi nne, inafuatiwa na AS Vita Club yenye tatu sawa na Simba, huku JS Saoura inaburuza mkia na pointi moja.
0 comments:
Post a Comment