Waziri Kangi Lugola amesema tayari serikali imepata majina ya wote waliohusika katika mauaji ya watoto Njombe.
Serikali imeahidi kuwachukulia hatua kali wale wote watakaobainika kuhusika katika mauaji ya watoto mkoani Njombe.
Watoto sita, wakiwemo watatu wa familia moja wenye umri chini ya miaka 10 wamepatikana wakiwa wamefariki katika mazingira ya kutatanisha mkoani humo.
Akizungumza Bungeni leo, Waziri wa Mambo ya Ndani nchini Tanzania, Kangi Lugola amesema tayari wameshabaini baadhi ya wale waliohusika na mauaji hayo na hatua kali zitachukuliwa.
"Uchunguzi wa awali unaonesha kuwa mauaji hayo yametokana na imani za kishirikina...n tayari tumeshawabaini baadhi ya wale ambao wameshiriki. Nawataka watu waache kuichezea serikali, tutaanza na mkoa wa Njombe," ameonya Lugola.
Lugola hata hivyo hakusema ni watu wangapi mpaka sasa wametiwa mbaroni kutokana na mauaji hayo.
Chanzo:Bbc
0 comments:
Post a Comment