Thursday, 31 January 2019

SIMBA YAMUUZA KICHUYA MISRI

...


Kichuya (kushoto) akiwa na Okwi

Baada ya jana klabu ya Simba kuweka wazi kuwa ipo kwenye mazungumzo ya mwisho na klabu ya Pharco ya Misri juu ya uhamisho wa Kichuya, hatimaye leo dili hilo limekamilika na Kichuya sasa si mchezaji wa Simba tena.

Akiongea na www.eatv.tv Mtendaji mkuu wa Simba Crescentius Magori amesema Kichuya amesaini mkataba wa miaka 4 na klabu hiyo pamoja na malipo mazuri ambayo hata Simba hawakuwa wanamlipa.

''Kichuya ni kijana wetu na klabu imefaidika naye sana hivyo tunafurahi amepata timu ya daraja la pili na itamlipa vizuri na sisi kama Simba tumepata maslahi mazuri kwahiyo tumemuuza'', amesema.

Kichuya ambaye alisajiliwa na Simba akitokea Mtibwa Sugar atacheza ligi kuu ya Misri licha ya kuwa amesajiliwa na Pharco ambapo kwa mujibu wa Magori ni kwamba tayari timu hiyo imemtoa kwa mkopo katika klabu ya Enppi inayoshiriki ligi kuu.

Tayari Kichuya amesharipoti katika timu ya Enppi na kesho Februari 1, 2019 ataanza mazoezi na timu yake ya Enppi kujiandaa na mchezo wa Ligi Kuu ya Misri dhidi ya Al Ahly utakaochezwa Jumanne Februari 5, 2019.

Enppi inashika nafasi ya 14 kati ya 18 zinazoshiriki ligi kuu. Timu hiyo imecheza mechi 20, imeshinda 4, sare 9 na kufungwa mechi 7.
Chanzo - EATV
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger