Kuelekeza mchezo wa 3 Kundi D ligi ya Mabingwa Afrika, klabu ya Simba kupitia kwa kocha wake Patrick Aussems, amethibitisha kuwa mshambuliaji wa timu hiyo John Bocco ameshapona na anatarajiwa kuanza kucheza muda wowote.
Akitoa ufafanuzi juu ya kutolewa kwenye michuano ya SportPesa, Aussems pia aligusia suala la Bocco na kuweka wazi kuwa maendeleo yake ni mazuri.
“Kuhusu mshambuliaji John Bocco yupo vizuri, anamalizi mazoezi mepesi ya mwisho na anaweza kucheza kabisa mechi yetu ijayo dhidi ya Al Ahly'', alisema Aussems.
Bocco aliumia kwenye mechi ya kwanza ya Kundi D dhidi ya JS Sauora iliyopigwa kwenye uwanja wa taifa Dar es salaam Januari 12.
Wachezaji wa Simba ambao bado wapo majeruhi ni Erastoi Nyoni aliyeumia kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi pamoja na Shomari Kapombe aliyeumia kwenye kambi ya timu ya taifa mwaka jana.
0 comments:
Post a Comment