Waziri wa Maji na Umwangiliaji Profesa Makame Mbarawa (mwenye kofia nyeusi) akiwa ameongozana na msimamizi wa miradi alipofanya ziara katika Kata ya Goba, Manispaa ya Ubungo manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam na kuwahakikishia wakazi hao kupatiwa maji ifikapo Februari Mosi mwaka huu. Picha zote na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.
Waziri wa Maji na Umwangiliaji Profesa Makame Mbarawa (mwenye kofia nyeusi) akipata maelezo toka kwa msimamizi wa miradi mara alipofanya ziara katika Kata ya Goba, Manispaa ya Ubungo manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Moja ya mita za maji ambazo zimeshasafungwa kwa wakazi wa Goba Kinzudi jijini Dar es Salam.
Waziri wa Maji na Umwangiliaji Profesa Makame Mbarawa (kulia) akijibu hoja za mkazi wa Goba Kinzudi jijini Dar es Salaam Waziri wakati alipofanya ziara katika Kata ya Goba, Manispaa ya Ubungo manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam na kuwahakikishia wakazi hao kupatiwa maji ifikapo Februari Mosi mwaka huu.
Mkazi wa Goba Kizudi jijini Dar es Salaam Waziri akitoa shukrani zake za pekee mbele ya wanahabari kwa Serikali jinsi ambavyo imepanga kuwapatia maji.
Waziri wa Maji na Umwangiliaji Profesa Makame Mbarawa (kulia) akijibu hoja za mkazi wa Goba Kinzudi jijini Dar es Salaam Waziri wakati alipofanya ziara katika Kata ya Goba, Manispaa ya Ubungo manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam na kuwahakikishia wakazi hao kupatiwa maji ifikapo Februari Mosi mwaka huu.
Mkazi wa Goba Kinzudi akimshukuru waziri kufika eneo lao na kusikiliza changamoto zao.
Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.
Serikali imewathibitishia wakazi wa kata ya Goba, Manispaa ya Ubungo manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam uhakika wa kupata maji safi na salama kuanzia Februari mosi Mwaka huu.
Akizungungumza baada ya kufanya ziara katika maeneo hayo, Waziri wa Maji na Umwangiliaji Profesa Makame Mbarawa amesema Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA ) imepeleka vijana wapatao 50 kukamilisha mradi wa usambazaji maji katika maeneo hayo.
Amesema vifaa vyote vimefikishwa katika eneo hilo na vijana wameanza kazi rasmi.
"Kuanzia Ijumaa Februari mosi maji katika maeneo haya yataanza kutoka na kila mwananchi atapata maji safi na salama hivyo naomba muendelee kuwa wavumilivu wakati shughuli ya uunganishwaji mabomba inaendelea," amesema Profesa Mbarawa.
Amesema katika mitaa ya Kinzudi na kwa Ubarikio zilizopo katika kata hizo wanatarajia kuunganisha wateja wapya mia saba (700) ambao wanatarajia kuongeza mapato ya DAWASA.
"Tunakiri kukosea kwa kuwa hakukuwa na haja ya mradi huo kuchelewa kutokana na kutekeleza miradi mingi kwa wakati mmoja na sasa tumekubaliana kuwekeza nguvu katika mradi mmoja na utakapokamilika tunahamia mwingine kwa wingi," amesema.
Kwa upande wao wakazi wa Mtaa hiyo wameishukuru serikali kwa kuwaahidi kupata maji kwani wamekuwa wakiteseka kwa kutumia muda mrefu kutafuta maji.
Mmoja wa wakazi hayo Juma Saidi amesema wamechimba mitaro ili wapatiwe huduma hiyo ambapo kwa sasa wanaishukuru DAWASA kuwatua mzigo huo.
"Huku kwetu maji yamekuwa ni lulu maana yanauzwa shilingi 500 kwa ndoo jambo linalotufanya kuhangaike hata kuyapata," amesema.
0 comments:
Post a Comment