Afisa mmoja wa polisi aliyeshtakiwa kwa madai ya kumuua mkewe pamoja na mtoto mwenye umri wa miaka 5 katika kambi ya maafisa wa kupambana na wezi wa mifugo eneo la Suswa Machi 2018, amejiua.
Cosmas Kipchumba Biwott, 27, ambaye alikuwa amesimamishwa kazi kwa muda, alijiua Jumanne, Januari 29 katika kituo cha polisi cha Nandi Hills alikozuiliwa kwa mashtaka ya wizi wa kimabavu.
Kulingana na habari zilituzofika katika meza yetu hapa TUKO.co.ke, Kipchumba alimwomba mlinzi wa selo alimokuwa kumsindikiza chooni majira ya saa sita na dakika 10 mchana mita 20 kutoka kwenye selo hiyo.
Wakiwa njiani, alikiokota kipande cha glasi/chupa na kukitumia kujirarua shingo.
Alivuja damu nyingi huku akilepelekwa katika hospitali ya Rufaa ya Kapsabet alikothibitishwa kufariki.
‘Njiani, mfungwa huyo aliokota kipande cha glasi na kujirarua shingo upande wa kushoto na kuanza kuvuja damu,’’ polisi walisema.
Wakiwa njiani, alikiokota kipande cha glasi na kukitumia kujirarua shingo.
Ilibainika kuwa Kipchumba alizuiliwa kituoni Jumatatu, Januari 28 kusubiri uchunguzi kuhusu kesi nyingine.
Alikuwa amefikishwa kortini awali lakini hakimu wa mahakama ya Kapsabet akatoa agizo la kuzuiliwa kwa muda.
Katika kisa kingine, inadaiwa kuwa Kipchumba alimuua mkewe Jane Njoki na mwanawe Shantel Nyambura.
Kulingana na ripoti ya polisi, Kipchumba alimpiga mkewe risasi 20 kabla kumgeukia mwanawe na kumuua vile vile.
Alifikishwa kortini lakini akaachiliwa kwa dhamana kabla kukamatwa tena kwa wizi wa kimabavu.
0 comments:
Post a Comment