Uongozi wa Simba umeshangazwa na tabia za mashabiki kuwalaumu viongozi baada ya kupoteza mchezo wa jana wa SportPesa Cup hatua ya nusu fainali kwa kufungwa bao 2-1 na Bandari ya Kenya.
Simba jana ilitolewa kwenye hatua ya nusu fainali ya michuano ya SportPesa na kuyeyusha mipango ya kucheza na Everton ya England pamoja na kupishana na fuko la fedha za mshindi wa kwanza zaisi ya milioni 60.
Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema mashabiki wa Simba na watani zao wamekuwa wakiwasema kwa maneno mazito ambayo si ya kiungwana hali ambayo kishabiki haina maana.
"Wengi wananivaa mimi na kunipa lawama ambazo sistahili kisa tumefungwa, mashabiki wanapaswa watambue kuwa mimi si mchezaji, siwezi kufunga kazi yangu kubwa ni kuhamasisha mashabiki pamoja na wachezaji kucheza kwa morali.
"Wanalalamika mara Niyonzima amekosa nafasi ya wazi mnataka mimi nifunge? Okwi ameshindwa kufunga mimi nifanye nini, najua tumefungwa michuano ya SportPesa Cup tunashindwa kucheza na Everton ila lawama na matusi tunashushiwa viongozi, mashabiki tubadilike ," alisema Manara.
Chanzo- Saleh Jembe blog
0 comments:
Post a Comment