Nyumba yake ambayo ipo Los Angeles Marekani ilivamiwa muda mchache tu baada yakushinda pambano lake dhidi ya Adrien Broner.
Ripoti iliyotolewa na Polisi wa mjini Los Angeles imeeleza kuwa nyumba hiyo ilivamiwa usiku wa Jumapili na wezi ambao hawakuweza kuiba chochote kutokana na wana usalama hao kuwahi eneo la tukio na kudhibiti hali hiyo.
Polisi wameeleza kuwa walitumiwa ujumbe juu ya kuwepo kwa wezi hao na mtu mmoja katika timu ya Pacquiao hivyo wakawahi kwa polisi.
Pacquiao alishinda pambano hilo dhidi ya Adrien kwa pointi na baada ya pambano hilo la (WBA world welterweight) akaweka wazi kuwa anahitaji kurudiana na bondia Floyd Mayweather ambaye alimpiga mwaka 2015.
Chanzo:Eatv
0 comments:
Post a Comment