Monday, 21 January 2019

KAULI YA LISSU KUVULIWA UBUNGE, CHADEMA WASHANGAZWA NA SPIKA

...
Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeamua kuingilia kati kufuatia kauli ya Spika wa Bunge wa Job Ndugai kusema Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu lissu anaweza kuondolewa Ubunge wake kufuatia kiongozi huyo kufanya ziara nchini Uingereza bila kibali cha Spika.

Akizungumzia kauli hiyo ya Spika Ndugai, Mkurugenzi wa Mawasiliano, Itikadi na Mambo ya Nje wa CHADEMA John Mrema amesema kauli ya Spika haina tija kwa kuwa Tundu Lissu bado hajapewa ruhusa na Daktari wake kurejea nchini kwa madai kuwa amepona kabisa.

Mrema amesema, "Spika si Daktari mpaka aseme kuwa Lissu amepona na hajawahi kumtembelea kwa kipindi chote tokea apelekwe hospitali. Tunakumbuka aliyewahi kuwa waziri wakati wa serikali ya awamu ya nne, Prof. Mwandosya aliugua kwa zaidi ya mwaka, lakini hatukusikia kauli za aina hii."
 
Akizungumza na baadhi ya vyombo vya habari jana, Spika Ndugai alimtaka Mbunge Tundu Lissu huyo kurejea nchini ili kuendelea na shughuli za Bunge kwa kuwa hana kibali cha kuwa nje ya nchi.

Spika Ndugai aliongeza Lissu hana ruhusa ya kuwa nje ya Bunge, hivyo anatakiwa kurejea nchini kuendelea na shughuli za ubunge.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger