Sunday, 6 July 2014

WANAFUNZI WA DODOMA UNIVERSITY WATOA TAMKO-KUHUSU SKENDO JUU YA UKAHABA,WASEMA KUWA WANAOFANYA BIASHARA HIYO HUTUMIA STATUS YA UDOM KUPATA WATEJA

...
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY


Mji wa Dodoma unakua kwa kasi kubwa, ofisi  za serikali na taasisi zisizo za kiserikali zinajengwa kwa wingi.



Wafanyabiashara nao hawapo nyuma wakiwamo wanaonadi miili yao kama bidhaa. Hawa ni maarufu kwa majina kama vile makahaba, machangudoa na dada poa.


Kimsingi, wauza miili wanavutiwa na mengi mjini Dodoma, ikiwamo ongezeko la watu linalosababishwa na kuwepo kwa taasisi za elimu ya juu.


Pia shughuli nyingi za kijamii na kitaifa zimekuwa zikifanyika mjini hapo, hivyo kuvutia watu wengi wakiwamo wafanyabiashara hawa.


Kushamiri kwa biashara ya ukahaba kumewafanya wahusika kutafuta ‘sumaku’ ya kuvutia wateja. 


Uchunguzi wa Mwananchi umebaini mojawapo ya njia wanazotumia kupata wateja ni kujinadi kuwa wao ni wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom).

Ni kwa sababu hii, chuo hicho ambacho kimsingi kimebadili maisha ya kijamii na kiuchumi ya mji wa Dodoma,  mara kwa mara kimekuwa kikikumbwa na kashfa ya wanafunzi wake kujihusisha na vitendo vya ukahaba.



Udom na ukahaba


Baadhi ya watu waliohojiwa wanasema makahaba wengi wanatumia jina la chuo hicho kama ‘ndoano’ ya kuwanasa wanaume.


 Na kwa hakika mkakati wao huu unaonyesha kufanikiwa, japo kwa upande mwingine umekuwa na matokeo hasi kwa jamii ya chuo hicho kinachoongoza kwa kuwa na wanafunzi wengi nchini.



Moja ya maeneo ya starehe ambayo makahaba hawa wamegeuza kuwa vijiwe vyao vya kawaida ni pamoja na klabu moja ya starehe maarufu iliyopo eneo la Makole.


Baadhi ya wateja waliohojiwa klabuni hapo  wanasema hawana uhakika wa wanafunzi kujihusisha na biashara hiyo, na kuwa maneno ya wanafunzi wa Udom kuhusishwa na  ukahaba yamekuwa katika midomo ya wakazi wengi mjini hapo, lakini bila ya kuwa na ushahidi.


Mmoja wa wateja ambaye hakupenda kujitambulisha jina lake, alisema upo uwezekano wa makahaba kutumia jina la chuo kwa minajili ya kushawishi mteja na kuficha utambulisho halisi



“Kahaba anajisikia ujiko (sifa) sana kujitambulisha kuwa ni mwanafunzi wa Udom kutokana na sifa ya chuo hicho kuwa na wasichana wazuri sana,” anasema. 

Kwakweli hata mimi binafsi nishawasikiaga mademu kibao ukikutana nao sehemu ukimuuliza tu we nani na wafanya nini now  utaskia tu ooh nasoma Udom then ukimuuliza mbona uko apa Dar na vyuo bado havijafungwa ataanza kujiumauma tu lol haa ahaaa TUMEWASTUKIAAA..
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger