Wapiganaji wa Al Shabaab
Bomu lililotegwa
kwenye gari limelipuka na kuua watu wanne karibu na Bunge la Somalia na
wengine kujeruhiwa, maafisa wa Polisi wamesema.
Habari zanasema bomu hilo lilipiga nje
ya lango kuu la kuingia katika majengo ya Bunge la Somalia baada ya askari kumrushia risasi mtu anayedaiwa kulipua bomu hilo.
Mshambuliaji aliyejitolea mhanga pia alikufa, alipolipua gari lake, baada ya kukataliwa kuingia kwenye eneo la bunge.
Kabla ya hapo, mshambuliaji huyo alijaribu kuingia katika wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi, lakini alizuiliwa.
Mlipuko mwingine uliofanywa na waasi hao katika majengo ya bunge mwezi Mei uliua watu 10.
Kundi la Al shabaab lilipoteza udhibithi katika mji mkuu wa Mogadishu tangu mwaka 2011 na tangu wakati huo limekuwa likiendesha mashambulizi ya mabomu na kufanya mauaji.
Mapema wiki hii Mbunge maarufu Ahmed Mohamud Hayd, aliuawa kwa kupigwa risasi katika mji huo, katika shambulio linalodaiwa kufanywa na Al Shabaab. CREDIT:MJENGWA
0 comments:
Post a Comment