Tuesday, 8 July 2014

SOMA KISA KIZIMA JINSI HOUSE GIRL ALIVYOMUUA BOSI WAKE KWA KISU-SINGIDA

...



SAKATA la wafanyakazi wa ndani kunyanyaswa na mabosi wao limeingia katika sura ya kipekee, safari hii mabosi wamegeukwa ambapo mmoja amedaiwa kuuawa na hausigeli wake aliyetajwa kwa jina la Valentina Karenge (17).

Ndugu wa marehemu akiuandaa mwili kwa ajili ya kuagwa
Hatua hiyo imekuja siku chache baada ya mfanyakazi huyo wa ndani mkoani Singida kudaiwa kumuuua tajiri yake kwa kumchoma kisu sehemu ya juu ya titi la kulia kwa madai ya kunyanyaswa naye.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida (SACP) Geoffrey Kamwela alisema tukio hilo la aina yake lilijiri saa 10 alfajiri Juni 29, mwaka huu eneo la Sabasaba, Kata ya Utemini, Manispaa ya Singida.
Kamanda Kamwela alimtaja marehemu kuwa ni Pendo Justine Kiula (24)  ambaye ni Karani wa Mahakama ya Wilaya ya Singida.
Ndugu,jamaa na marafiki wakitoa heshima za mwisho kwa marehemu, Pendo Justine Kiula.
“Baada ya marehemu kuchomwa kisu na msichana wake huyo, alitoka nje ya nyumba na kukimbilia kwa majirani kwa ajili ya kuomba msaada lakini wakati majirani wakiwa katika harakati za kumpeleka hospitali, alianguka chini na kufa papo hapo,” alisema Kamanda Kamwela.
Alisema baada ya polisi kuendesha msako kwa kushirikiana na raia wema hatimaye walifanikiwa kumkamata msichana huyo majira ya saa 8 mchana uliofuata maeneo ya Uwanja wa Ndege akiwa katika harakati za kutoroka.
.....wakiendelea kuaga mwili wa marehemu.
Naye Naomi Abrahaman ambaye ni mpangaji mwenzake marehemu, alisema kabla ya tukio hilo walikuwa pamoja jioni na kushiriki chakula cha jioni na kisha wakaenda kulala.
Alisema ilipofika saa kumi kasoro usiku, alishituka kugongewa mlango na marehemu na alichokisikia akikizungumza ni;  Kwa jina la Yesu nakufa, kwa jina la Yesu nakufa.’
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida (SACP) Geoffrey Kamwela akitoa ufafanuzi kuhusu kesi hiyo ya mauaji.
“Alipiga mlango wangu kwa nguvu na damu zilikuwa zikimvuja, akaenda kwenye chumba kingine cha mpangaji akapiga tena mlango huku akisema jamani nisaidieni nakufa, kwa jina la Yesu nakufa, akaanguka.
“Nilipotoka chumbani, nilimkuta ameanguka chini huku akiwa ameshikilia pale alipochomwa kisu huku damu zikiendelea kumtoka.” Alisema mpangaji huyo.
Huu ni mfano wa kisu kilichotumika katika mauaji hayo.
Akaendelea: “Kumbe mtuhumiwa alimchoma kisu wakati chumb     ani kukiwa na giza, baada ya kufanya tukio hilo alikimbia nasi tukawa tunaogopa kuingia chumbani kwa kuhofia pengine kunaweza kukawepo mtu aliyejibanza ndani ya chumba hicho.”
Marehemu alizikwa Julai 2, mkoani Singida. Ameacha mtoto mmoja.
Mungu ailaze mahali pema peponi roho yake. Amina.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger