KOCHA Mkuu mpya wa Yanga, Mbrazili, Marcio Maximo, jana alianza kazi yake kwa mkwara mzito huku kila aliyehudhuria akionyesha kutikisa kichwa kuikubali.
Wachezaji
wa Yanga wakiongozwa na kocha msadizi, Leonado Martins (wa kwanza
kushoto) kwenye mazoezi ya timu hiyo yaliyofanyika jana Coco.
Maximo majira ya saa mbili kamili asubuhi alikwishatua kwenye Ufukwe
wa Coco jijini Dar es Salaam na kuanza rasmi mazoezi na timu hiyo ya
Jangwani na kuwakusanya tena wachezaji wake saa tisa kamili kwenye
Uwanja wa Bandari Tandika kwa mazoezi ya takribani saa mbili.Maximo ambaye amekuwa akifanya mambo yake kisasa, alianza kama kawaida yake huku akiwasimamia wachezaji wake kunyoosha viungo na baada ya hapo kuanza kuwakimbiza.
Wachezaji wa Yanga ambao wengi walikuwa wametoka kwenye mapumziko, walikimbizwa kwa umbali wa kilomita 1.5 mara mbili kwenda na kurudi huku kocha huyo akiungana nao akiwa na kocha wa vijana, Salvatory Edward.
Kocha wa Yanga, Mbrazil, Marcio Maximo akisimamia leo Coco Beach.
Maximo alionyesha kuwa yupo fiti pamoja na kwamba umri umeenda baada
ya kuanza na wachezaji hao na kumaliza nao mbio bila kupumzika sehemu
yoyote ambapo walitumia dakika 30.Mara baada ya kumaliza kukimbia, wachezaji wa Yanga walitakiwa kupumzika kwa kunywa maji na kunyoosha viungo na kuanza zoezi la kuruka koni na kukimbia mbio fupi ambazo zilichukua dakika 30, msimamizi akiwa ni kocha msaidizi, Leonardo Neiva.
Kama ilivyo kawaida yake, Maximo aliendelea na utani wake huku akichombeza kwa maneno ya Kiswahili; tupo pamoja, harakaharaka, ongeza mwendo, usichoke na mengine mengi.
Baada ya kumaliza kuruka koni, Maximo alionyesha kuridhika na kuwaita pamoja na viongozi wengine waliokuwepo uwanjani hapo na kuzungumza nao.
Coutinho (juu) akifanya mazoezi na beki Yusuf Ngao.
Baada ya mazungumzo kocha huyo aliwakusanya wote na kuomba dua na
kutawanyika ambapo aliwapa ruhusu ya kuzungumza na waandishi, lakini
yeye akapanda prado lake na kutimka.Hata hivyo, saa tisa alasiri kocha huyo alilianzisha tena na mastaa wake kwenye Uwanja wa Chuo cha Bandari, Temeke ambapo alianza kwa kuwazungusha uwanja raundi tatu huku kukukiwa na mashabiki kibao.
Mashabiki hao walishuhudia mazoezi mazuri huku kocha huyo akiwataka wachezaji wake kufanya kila kitu kwa uhakika.
Mashabiki waliofurika uwanjani hapo walionekana kushangilia kwa nguvu kubwa kila Mbrazili Coutinho alipokuwa akigusa mpira na wakati Maximo alipokuwa akiwafokea wachezaji wake pale walipofanya vibaya.
Kocha Maximo akimuelekeza jambo mshambuliaji Jerry Tegete.
Mashabiki waliokuwepo uwanjani hapo walionekana kumsifia kocha huyo,
huku wengi wakiamini kuwa kama ataendelea hivyo, Yanga itakuwa bonge la
timu.Maximo aliongoza mazoezi hayo kwa ustadi wa hali ya juu, huku msaidizi wake naye akiwa moto kwenye kila kitu ikiwa ni pamoja na kukimbia, kupiga pasi na kukaba.
Hata hivyo, Coutinho kuna muda alidondoka na kuchubuka mguuni, lakini bado aliendelea kukipiga hali iliyowafanya mashabiki washangilia.
Kiungo mpya wa Yanga, Mbrazil, Coutinho (7) akipasha na wenzake.
Mazoezi ya jioni yalikamilika saa 11:45 jioni na kukamilisha saa nne
za Maximo za siku ya kwanza, huku Coutinho akifunga mabao mawili.Wachezaji wa kikosi cha kwanza waliohudhuria mazoezi ya jana ni Juma Kaseja, Ally Mustapha ‘Barthez’, Juma Abdul, Salum Telela, Hussein Javu, Said Bahanuzi, Omega Seme, Rajab Zahiri, Mbuyu Twite na Saleh Abdallah pamoja na wa kikosi cha pili..
0 comments:
Post a Comment