Monday, 21 January 2019

TAKUKURU YAZIANIKA IDARA ZINAZOONGOZA KWA RUSHWA SHINYANGA

...
Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa mkoa wa Shinyanga imetoa taarifa ya utendajikazi wake kuanzia mwezi Oktoba hadi Desemba 2018,katika kuchunguza,kuelimisha umma na kufanya utafiti,kwa mujibu wa sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa Na.11 ya mwaka 2017. 

Taarifa hiyo imeonyesha kupokea taarifa 90 ambapo idara ya polisi(10), elimu(12), mahakama(11), serikali za mitaa(10), ardhi(10), afya(7) na huduma za kifedha(7) zikitajwa kulalamikiwa kwa vitendo vya rushwa. 

Akitoa taarifa hiyo kwa vyombo vya habari kaimu mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Shinyanga Francis Luena alisema ofisi hiyo imetembelea miradi 9 yenye thamani ya shilingi bilioni 5.424 na kubaini baadhi ya miradi kuwa na dosari. 

“Miradi yenye dosari ni pamoja na mradi wa machinjio na banda la kuanikia ngozi wilaya ya kishapu ambao thamani yake ni shilingi milioni 12, fedha zinazochunguzwa ni shilingi milioni 4.3, pamoja na mradi ujenzi wa kituo cha mabasi baada ya kuufuatilia iligundulika shilingi milioni moja matumizi yake yalikuwa hayaeleweki,” alisema Luena. 

Kaimu Mkuu huyo alisema kesi zinazoendelea mahakamani ni 19 na kwamba taasisi hiyo imejipanga kuendelea kutoa elimu kwa watumishi mbalimbali, kufanya uchunguzi wa vitendo vya rushwa na kwafikisha mahakamani wahusika. 

Na Malaki Philipo – Malunde1 blog
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger