Monday, 21 January 2019

ODINGA AMKUMBUKA BABA YAKE MZAZI ASEMA ALIKUWA JASIRI

...
Kiongozi wa ODM Raila Odinga Jumapili, Januari 20 
aliadhimisha kumbukumbu ya miaka 25 ya kifo cha baba yake mzazi Jaramogi Oginga Odinga 


Oginga alikuwa mwanasiasa maarufu sana katika kupigania uhuru wa Kenya, na aliaga dunia Januari 20 1994. 


Kupitia mtandao wa kijamii, Raila alimtaja baba yake kuwa mtu jasiri, aliyejali wengine na aliyefanikisha kupatikana uhuru wa nchi ya Kenya. 

"Miaka 25 tangu ulipotuacha. Lakini vitendo vyako vya kijasiri na kujitolea bado vinaendelea kutupa motisha Kenya na mamilioni barani Afrika.Leo tunakukumbuka Jaramogi," ulisoma ujumbe huo. 

Baba ya Raila atakumbukwa sana kwa kuwa makamu wa kwanza wa rais baada ya Kenya kupata uhuru na alikuwa ofisini kati ya 1964 na 1966. 

Kinachoshangaza ni kwamba, baba na mwana wana vitu vingi vinavyolingana katika siasa zao. Itakumbukwa Raila alikiongoza kikosi cha kupinga katiba iliyokuwa imependekezwa na alama yao ilikuwa ‘No’ na nembo ya chungwa. 

Alipokuwa makamu wa rais, Jaramogi alipinga vitu kadhaa alivyotaka Jomo Kenyatta, aliyekuwa akiegemea sana mataifa ya Magharibi. 

Yeye ndiye aliyeanzisha kauli maarufu ya "Bado Uhuru” (Not Yet Uhuru) ambacho pia ni kichwa cha kitabu kuhusu maisha yake. 

Raila, wakati akiwa waziri wa barabara na baada ya kuongoza kampeni za kura ya maamuzi na kushinda, alianzisha chama cha Orange Democratic Movement (ODM), alivyofanya baba yake akianzisha chama cha Kenya People's Union (KPU) alipokuwa haelewani na Jomo Kenyatta.


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger