Wakati Misri imekuwa nchi ya kwanza ya kiarabu kuruhusu uzalishaji na uuzaji wa dawa yenye kazi ya kuongeza hisia za tendo la ndoa kwa wanawake, Mwandishi wa BBC Sally Nabil anachunguza soko lake katika nchi hiyo yenye kufuata maadili ya kidini zaidi.
"Nilihisi nimechoka na kizunguzungu, na moyo wangu ulikuwa ukipiga mbio."
Hivi ndivyo Leila alivyohisi baada ya kuchukua kidonge chake cha kwanza kinachojulikana kama "Viagra ya kike" - lakini huitwa flibanserin.
Dawa hii ilikuwa ya kwanza kuidhinishwa kwa matumizi nchini Marekani karibu miaka mitatu iliyopita, na sasa inazalishwa Misri na kampuni ya dawa ya ndani.
Leila - si jina lake halisi - ni mke mwenye imani ya kihafidhina na ana miaka 30 na zaidi.
Anapenda zaidi kuficha utambulisho wake, kama wanawake wengi Misri, kwani kuzungumza juu ya matatizo ya ngono na mahitaji ya ngono bado ni mwiko.
Baada ya takriban miaka 10 ya ndoa, anasema aliamua kutumia dawa hizo "kama sehemu ya udadisi tu".
Leila, ambaye hana matatizo ya afya, alinunua dawa bila kupata mwongozo wa mtaalamu - jambo la kawaida sana huko Misri, ambapo watu wanaweza kununua dawa nyingi madirishani tu.
"Muuza dawa aliniambia nipate kidonge kila usiku kwa wiki chache." Alisema kuwa hakutakuwa na madhara, "anasema.
"Mimi na mume wangu tulitaka kuona nini kitatokea. Nilijaribu mara moja, na kamwe sitafanya tena."
Viwango vya talaka vinaongezeka nchini Misri, na ripoti za vyombo vya habari vya ndani vimehusisha kuwepo kwa matatizo ya ngono endelevu kati ya wanandoa.
Mtengenezaji wa ndani wa dawa hiyo ya flibanserin anasema wanawake watatu kati ya kila 10 nchini Misri wana hisia za viwango vya chini vya ngono.
Lakini takwimu hizi ni makadirio ya kawaida - takwimu hizo ni vigumu kupatikana nchini humo.
"Tiba hii inahitajika sana hapa - ni mapinduzi," anasema Ashraf Al Maraghy, mwakilishi wa kampuni hiyo.
Via BBC
0 comments:
Post a Comment