Makambo, Ajibu na Tambwe.
Mshambuliaji mkongwe wa klabu ya Stand United ambaye pia ni nahodha wa kikosi hicho, Jacob Masawe amezitahadharisha timu zitakazokutana na Yanga kuwa wasidharau kwani timu hiyo ni bora.
Ametoa tahadhari hiyo baada ya mchezo wa jioni hii ambapo yeye ameibuka shujaa kwa kufunga goli pekee la ushindi kwa Stand United na kumaliza mbio za Yanga kucheza mechi 19 bila kufungwa.
'Licha ya sisi kushinda lakini ukweli ni kwamba Yanga ni timu bora na ina wachezaji bora hivyo kila timu inayokutana nao isiwabeze bali icheze kiushindani'', amesema.
Kuhusu bao lake alilofunga kwa kichwa dakika ya 88 ya mchezo, Jacob Masawe amesema ni zawadi kwa mashabiki wao ambao walifurika kwenye uwanja wa Kambarage na kuwapa nguvu mwanzo mpaka mwisho wa mchezo.
Yanga sasa imepoteza mechi 1 katika mechi zake 20 ilizocheza huku ikiwa imetoa sare 2 na kushinda mara 17 hivyo kujikusanyia alama 53 ikiwa kileleni mwa msimamo wa ligi.
Stand United wamefikisha alama 25 na kupanda kwa nafasi kadhaa wakitoka 16 hadi 12 kwenye msimamo wa ligi kuu wakiwa wamecheza mechi 23.
0 comments:
Post a Comment