Monday, 21 January 2019

CAG AHOJIWA ZAIDI YA SAA TATU DODOMA

...
Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge imetumia zaidi ya saa tatu kumhoji Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG), Prof.Mussa Assad kufuatia wito wa Spika Job Ndugai kumtaka kufika kwenye kamati kutokana na kauli yake ya kuliita bunge dhaifu.

Prof.Assad ameanza kuhojiwa 5:06 asubuhi na mahojiano yake yalihitimishwa saa 8:47 mchana.

Awali baada ya kuingia kwenye ukumbi Prof.Assad alitoka nje ya ukumbi saa 6:45 mchana akisubiri kamati ikijadili hoja zake na mwenendo wa mahojiano ili kama kuna haja ya kufafanua aitwe tena.

Baadate ameitwa saa 7:15 mchana na kutoka 7:57 mchana ambapo alikaa kwa muda kusubiri kuitwa tena saa 8:35 mchana kuelezwa uamuzi wa shauri lake.

Kamati hiyo ilimaliza mahojiano naye saa 8:47 mchana chini ya Mwenyekiti wake Emmanuel Mwakasaka.


“CAG Prof. Assad amefika leo mbele ya kamati baada ya wito aliopewa na Spika na tumemhoji. Sisi kwa kanuni zetu hapa tunamwita mtuhumiwa, tukishakamilisha hili suala tunalipeleka kwa Spika wa Bunge, Job Ndugai,” amesema Mwakasaka.

Aidha, Mwakasaka amesema Prof. Assad ameonyesha ushirikiano mkubwa kwa maswali aliyoulizwa kamati hiyo.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger