Wednesday, 19 December 2018

POLISI WATOA AMRI YA KUKAMATWA KWA MKE WA RAISI MSTAAFU NI BAADA YA KUMPIGA MWANAMITINDO

...

Polisi nchini Afrika Kusini imetoa amri ya kukamatwa kwa Grace Mugabe, mke wa aliyekuwa rais wa Zimbabwe Robert Mugabe ambaye anatuhumiwa kumshambulia na kumjeruhi mwanamitindo wa Afrika Kusini, Gabriella Engels, mwaka 2017.

Mwanasheria anayefanya kazi na shirika la kutetea haki za binadamu la AfriForum la huko Afrika Kusini, Garrie Nel amesema amethibitishiwa na Polisi kuhusu kutolewa kwa amri hiyo, na kuongeza kuwa ikiwa Bi. Mugabe atakanyaga kwenye ardhi ya Afrika Kusini atakamatwa.

Mwanasheria huyo vile vile ametaka mchakato wa kumtia mbaroni Grace Mugabe na kumsafirisha hadi Afrika Kusini uanze sasa.

Grace Mugabe anatuhumiwa kumpiga na kumjeruhi mwanamitindo Gabriella Engels kwenye hotel moja mjini Johannesburg Agosti mwaka 2017, lakini hakushtakiwa kwa sababu alikuwa na kinga ya kidiplomasia.
chanzo:Eatv
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger