Sunday, 30 December 2018

CHADEMA WAZUIWA KUFANYA MKUTANO JIMBONI KWA MBOWE

...
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimezuiwa kufanya mkutano pamoja na ziara ya viongozi wa chama hicho kitaifa, wilayani Hai mkoani Kilimanjaro.

Hayo yamebainishwa kupitia barua iliyotumwa kwa Katibu wa CHADEMA wilayani Hai, ambayo imesainiwa na Katibu tawala wa wilaya hiyo, Said Omary iliyoelekeza kusitisha kibali cha kufanya mkutano wilayani humo.

"Nimeagizwa na Mkuu wa Wilaya ambae ni mwenyekiti wa kamati ya usalama ya Hai. Nikuandikie kukutaka kusitisha mkutano na ziara ya viongozi wako kitaifa, tarehe 29/12/2018 na kuendelea", imesema barua hiyo.

Baada ya zuio hilo, Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya amethibitisha kukamatwa kwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Dkt. Vincent Mashinji pamoja na viongozi wengine watatu kwa makosa ya kufanya kusanyiko bila kibali.

Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger