Saturday, 29 December 2018

JUMA NKAMIA AKOMAA MUDA WA UBUNGE UWE MIAKA 7

...

Mbunge wa Jimbo la Chemba kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Juma Nkamia amesema kwa 2019 ataanza upya mpango wa kuwasilisha hoja yake ya kufanyika kwa uchaguzi kila baada ya miaka 7, licha ya kubainisha atakutana na ukosoaji mkubwa kutoka kwa baadhi ya wabunge wenzake.

Kwa mujibu Nkamia mwaka 2019 atahakikisha anazungumza na viongozi wa chama chake cha CCM ili kupata baraka juu ya kuendelea na mpango wake huo juu ya kuendelea au kutoendelea na baadaye kufuata taratibu za kibunge ili suala hilo liweze kujadiliwa ndani ya bunge.

Juma Nkamia amesema msimamo wake kuhusu kuwasilisha hoja ya ukomo wa miaka 7 bado upo palepale na kudai wanaokosoa ni wenye kutaka nafasi ya utawala mapema.

"Msimamo wangu kuhusu miaka 7, uko palepale Mungu akijalia tukiwa hai tutazungumza na chama changu na mamlaka za Bunge kwa mujibu wa taratibu wakiniruhusu nitaupeleka, nilishasema tangu mwanzo. Ila unajua wapingaji wa hoja zangu ni wanaotaka Ubunge haraka na Urais haraka, kiufupi mimi kama unavyonifahamu nikiamua jambo huwa sikwepeshi."

Mwaka 2017 Mbunge huyo wa Chemba alitaka kuwasilisha Bungeni Mswada wa kutaka kusogezwa kwa muda wa kufanya uchaguzi kutoka miaka 5 ya sasa hadi miaka 7 kwa kile alichokidai kuwa nchi imekuwa ikiingia kwenye gharama nyingi za kufanya uchaguzi wa mara kwa mara.

Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger