Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli ameagiza vikokotoo vya mafao ya wafanyakazi katika mifuko ya hifadhi ya jamii, vilivyokuwa vinatumika kabla ya mifuko kuunganishwa viendelee kutumika kwa kila mfuko hadi mwaka 2023
Tazama hapo chini nukuu ya maneno yote aliyoyasema leo
1. Nimewasikiliza, kimsingi lina umuhimu, na ndio maana nimeona niwaite, na hasa kwa sababu nimekuwa nikisikiliza maelezo hata ya regulator, yanakuwa too academic.
2.Ukishatoa maelezo ambayo ni too academic, unaelezea wastaafu, na kustaafu ni sifa na heshima, ulifanya kazi yako kwa uadilifu mkubwa, umesacrafice maisha yako kwa ajili ya kazi.
3. Unapoona hiyo heshima inakuwa karaha, mateso, inafrustrate kwa mfanyakazi yoyote, sasa mimi siko hapa kumfrustrate mtu, kwani hata mimi nilikuwa mfanyakazi.
4.Tuliamua kuunganisha mifuko, tulikubaliana NSSF ufanyiwe marekebisho, hatua hii ilitokana na ombi la muda mrefu la vyama vya wafanyakazi waliotaka hii mifuko iunganishwe.
5.Mifuko ya jamii yote ilikuwa na hali mbaya, kwa sababu haikuwa coordinated, waendesha mifuko wote walikuwa wanapigana vita, wanagombania wanachama, walikuwa hawapendani.
6.Mingine ilikuwa ikiendeshwa kiajabu, pakawa panaanzishwa miradi ya kiajabu, na miradi mingi ilikuwa ya majengo, nenda Kigamboni kaangalie yale majengo ya ndege vilaje, its a huge thing'.
7.Tulipongia madarakani tulikuta deni trilion 1.2, serikali yenyewe haijachangia hii mifuko, waliostaafu kwa wakati ule ilikuwa ni shida, kwani hata ile michango ya serikali haitekelezwi.
8.Tukaanza kulipa madeni, mpaka mwezi Machi mwaka huu madeni yote yalikuwa yamemalizika kulipwa.
9.Matatizo yapo lazima tuende kwenye solution, kile kikokotoo angalau imefika 50%, lakini pia hata hawa walioko chini ilifaa ipande, hata hiyo formula inachanganya zaidi.
10.Mishahara mingi ya wafanyakzi serikalini si mizuri, anapofika mwisho unampa kidogo kidogo haingii, si unipe tu yote nikafie mbali, nilipokuwa nachangia hukuniambia, leo nachukua unaniambia nachukua kidogo, hata logic haingii.
11.hata hawa Mawaziri, wabunge wanachukua hela yao yote, halafu uwaambie utachukua kidogo kidogo kila ukija, hawatakubali, kwenye reality, hata mimi hainingii.
12.Tunahitaji watu wetu wapate fedha nyingi walipwe, lakini pia tunahitaji huu mfuko usife, hii formula haipo duniani, mtu anamaliza halafu kiwango chake unakizidisha mara 4, haipo.
13. Walioweka formula hii ni makatibu wakuu wa wakati ule, wa wakati wangu hawawezi, kwa sababu kwenye ile mifuko wengine ni beneficiary, ni kosa walifanya.
14. Hifadhi za jamii zipunguze matumizi ya hovyo, kama mtu anastahili kulipwa 60% hatuwezi kumlipa kwa sababu hifadhi zinafanya matumizi ya hovyo.
15. Kwa mfano kuna mfuko mmoja unachapisha kalenda kwa 1.3 bilion, hiyo hiyo imeajiri walinzi ambao ni very expensive, wanawalipa bilioni 2 kwa mwaka, wakati wangeajiri SUMA JKT wangewalipa chini ya bilioni 1 kwa mwaka.
16. Uwekezaji kama ule wa Dege Heko village haufai, ukatumia fedha za wanachama bila ridhaa zao, halafu leo wastaafu uwaambie hamna hela formula imekataa.
17. Mifuko muweke utaratibu mzuri, ni suala ambalo haliingii akilini nikasubiri mpaka nitakapofika miaka 60 ndio nipate mafao yangu, nimetoa michango yangu, kwanza hayupo atakaye nikumbuka kama nilifanya kazi, hata contructor atakuwa kashakwenda kwao.
18. Kustaafu sio dhambi, kustaafu ni heshima, lazima awe respected, mwalimu amefundisha ameharibu na macho kutokana na chaki, halafu umpe condition.
19.Mazungumzo yenu yote nimeyasikia, mimi nimeamua, angalau tuwe na kipindi cha mpito, kikokotoo kilichokuwa kinatumika kwa kila mfuko kabla ya mifuko kuunganishwa, tuendelee katika kipindi cha miaka ya mpito.
20. Mtu anayestaafu anatakiwa kuheshimiwa, amelitumia taifa hili, amesacrafice, ni shujaa, kustaafu bila kufukuzwa ni heshima, hatakiwi kupata shida, nimeamua kikokotoo kiendelee katika kipindi hiki cha mpito, ambapo ni hadi mwaka 2023.
21. Mifuko hiyo itakuwa imetengamaa, ni matumaini yangu, nitaichungulia kweli kweli hiyo mifuko, na Waziri natoa maagizo yake, wachungulie kweli, ili kusudi watu wasitumie hovyo hovyo, hii ni mifuko ya wanachama.
22.Formula nzuri ni zile zinazo wapromote wafanyakazi, ndio ninazozitaka mimi, formula zinazowanyima haki wafanyakazi sio formula nzuri, ninashukuru katika kipindi hiki kifupi cha kuunganisha mifuko tumeanza kuona matokeo.
0 comments:
Post a Comment