Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameagiza kuendelea kutumika kwa kikokotoo kilichokuwa kinatumika zamani.
Rais Magufuli ametoa uamuzi huo leo tarehe 28 Desemba 2018 alipokutana viongozi wa vyama vya wafanyakazi nchini, watendaji wa mifuko ya hifadhi ya jamii na mawaziri wa wizara husika, kwa ajili ya kujadili masuala yahusuyo mafao ya wafanyakazi ikiwemo kuhusu kanuni mpya ya kukokotoa mafao ya wastaafu.
Vyama vilivyokutana na kuzungumza na Rais Magufuli ikulu jijini Dar es Salaam, ni pamoja na Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania(TUCTA), vyama shiriki, Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (PSSD na NSSF) na Mamlaka ya Usimamizi wa Hifadhi ya Jamii (SSRA).
Kanuni mpya ya kikokotoo iliyotolewa hivi karibuni na serikali, ambayo inaelekeza wastaafu kulipwa mkupuo wa asilimia 25 ya mafao pindi watakapostaafu na asimilia 75 inayobaki watakuwa wakilipwa kama pensheni ya kila mwezi.
Baada ya kikokotoo hicho kutangazwa kwa umma, baadhi ya vyama vya wafanyakazi ikiwemo TUCTA, viliipinga kanuni hiyo kwa maelezo kwamba inakandamiza wafanyakazi.
0 comments:
Post a Comment