Monday, 24 December 2018

BASATA YAWALEGEZEA ADHABU DIAMOND NA RAYVANNY...YAWAFUNGULIA KUPIGA SHOW NJE YA NCHI

...
Baraza la Sanaa la Taifa (Basata), limemruhusu msanii Naseeb Abdul ‘Diamond’ na Raymond Mwakyusa ’Rayvanny’ kufanya maonyesho yao nchini Kenya na Comoro ingawa rufaa yao itajadiliwa Februari mwakani.

Katika ratiba zake, Diamond na wasanii wake wataendelea na onyesho la Tamasha la Wasafi ambapo leo Desemba 24 watakuwa katika mji wa Embu, kabla ya kuhamia jiji la Mombasa Desemba 26 na kuelekea Comorro kwa shoo ya Desemba 28 na kumalizia Nairobi Desemba 31, 2018.

Diamond na Rayvanny walifungiwa Desemba 18, 2018 kutofanya maonyesho ndani na nje ya nchi kwa muda usiojulikana wakituhumiwa kufanya makosa mbalimbali tangu kuanza kwa Tamasha la Wasafi ikiwemo kuimba wimbo wa Mwanza ambao umefungiwa.

Pamoja na hilo siku tatu zilizopita waliendelea kutangaza kuendelea na maonyesho hayo pamoja na Basata kueleza hawajawaruhusu.

Katibu wa baraza hilo, Godfrey Mngereza amesema sababu ya kuwaruhusu ni baada ya kikao kilichoketi leo na kujadili maombi yao kuomba kusamehewa huku moja ya jambo walilolibaini ni kwamba wasanii hao walikuwa wameshaingia mkataba wa kufanya maonyesho hayo kabla ya kupewa adhabu.

“Pia kwa kuzingatia mahusiano mazuri kati ya nchi yetu na nyingine na athari kwa mashabiki wa nchi hizo ambao tayari walishakata tiketi za maonyesho hayo, Basata imewaondolea katazo la maonyesho hayo ya nje na kubakiza katazo la ndani ya nchi hadi pale Diamond na mwenzake Rayvany watakapoonyesha mabadiliko chanya kitabia,” amesema

Wakati kuhusu kukata rufaa, Mngereza amekiri wameipokea na kueleza wamewasiliana na mwenyekiti wa bodi ambapo suala lao hilo litajadiliwa kwa kina katika kikao cha kawaida cha bodi cha Februari 5 mwakani.

Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger