Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu
amewataka watendaji wa Serikali na Sekta ya Afya kuwajibika ipasavyo
kwa kutoa taarifa sahihi juu ya idadi ya wagonjwa wa kipindupindu
nchini.
Akitoa
tamko kuhusu mwenendo wa ugonjwa wa kipindupindu nchini pamoja na
tahadhari ya ugonjwa wa Zika jana jijini Dar es salaam Mhe. Ummy
alisema kuwa watendaji watakaoficha taarifa za wagonjwa katika maeneo
yao watawajibishwa.
“Mojawapo
wa changamoto katika mapambano ya kudhibiti mlipuko huu wa kipindupindu
ni utoaji wa idadi pungufu au kutotoa kabisa taarifa za wagonjwa wa
kipindupindu hivyo kupelekea kutokuwa na mafanikio katika mikakati
iliyowekwa” alisema Waziri Ummy.
Aidha,
alitoa wito kwa sekta nyingine kushirikiana na Wizara kupambana na
ugonjwa huo ili kukabiliana na baadhi ya changamoto zinazowakabili
watoa huduma za afya na elimu walioko katika maeneo mbalimbali nchini.
“
Jukumu la kupambana na mlipuko wa ugonjwa huu si la Wizara ya Afya
pekee naomba sekta nyingine ikiwemo Maji, Miondombinu, Biashara Elimu
na Mazingira tushirikiane kwa pamoja ili kuutokomeza ugonjwa huu”.
Mbali
na hayo Mhe. Ummy alieleza kuwa takwimu za kuanzia tarehe 1 hadi 7
februari mwaka huu zinaonyesha kuwa idadi ya wagonjwa wa kipindupindu
imepungua kutoka 459 ya wiki iliyoisha tarehe 31 Januari hadi 258 ambapo
ni sawa na punguzo la asilimia 44%.
Hata
hivyo Wizara imewatoa hofu wananchi na kuwakumbusha kuendelea kuchukua
tahadhari dhidi ya ugonjwa wa Homa ya Zika pamoja na magonjwa mengine
yanayoenezwa na Mbu.
0 comments:
Post a Comment