TAREHE 20/02/2016
-------------
-------------
Dondoo Alizozungumza Waziri Nape Nnauye;
Napenda
kuwafahamisha kuwa kufuatia Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la
Utangazaji Tanzania (TBC) kumaliza Muda wake, uundwaji wa Bodi Mpya
umekamilika.
Ni
vyema kuwafahamisha kuwa katika utaratibu wa kisheria wa kuunda Bodi ya
TBC mwenye Mamlaka ya kisheria ya Kumteua Mwenyekiti wa Bodi ni Rais wa
Jamhuri ya Muugano wa Tanzania.
Napenda
kutumia fursa hii kumshukuru sana aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya TBC
iliyomaliza muda wake, Prof. Mwajabu Possi na wajumbe wake wote kwa kazi
waliyoifanya kwa muda wote wa uhai wa bodi hiyo.
Ninaamini
Bodi Mpya itaendeleza yale mazuri yote yaliyofanyika na Baodi iliyopita
na kubuni mambo mengine mapya ili kuongeza tija kwa Shirika.
Baada ya kutoa maelezo haya ya awali, sasa nichukue fursa hii kuwajulisha yafuatayo;
1.
Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli amemteua Mhe. Balozi Herbert E.
Mrango (pichani) kuwa Mwenyekiti Mpya wa Bodi ya TBC. Uteuzi huu unaanza
tarehe 19/02/2016 kwa kipindi cha miaka Mitatu.
Balozi
Mrango kielimu ana shahada ya Uzamili katika uendelezaji wa Mifumo (MSc
– Systems Development) aliyoisomea Chuo Kikuu cha Dublin Nchini
Uingereza. Aidha amehitimu Shahada ya kwanza ya Takwimu za Kiuchumi
katika Chuo Kikuu Cha Dar Es Salaam, Tanzania.
Balozi
Mrango alishashika nyadhifa mbalimbali, zikiwemo kuwa Katibu Mkuu wa
iliyokuwa Wizara ya Miundombinu Kuanzia Februari, 2011 hadi September,
2013.
Nachukua
fursa hii kumpongeza Mhe. Balozi Mrango kwa kuaminiwa na Mhe. Rais wa
Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kushika wadhifa huu muhimu.
Aidha
nimhakikishie Mwenyekiti huyu Mpya wa TBC kwamba kwa kuwa Shirika la
TBC liko chini ya Wizara yangu, tutampa ushirikiano wa kutosha ili
kuendelea kuleta mabadiliko chanya katika shirika letu la Utangazaji.
2.Kwa
mujibu wa Sheria iliyounda TBC, baada ya Mhe. Rais kumteua Mwenyekiti
wa Bodi, Waziri mwenye dhamana na shughuli za utangazaji, anateua
Wajumbe sita wa Bodi.
Katika
uteuzi wa wajumbe wa Bodi ya Shirika la Umma, Ofisi ya Msajili wa
Hazina ilishatupatia vigezo vya utaalamu wa wajumbe wakati wa uteuzi.
Hivyo
basi, mimi Nape Moses Nnauye, nikiwa Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa
na Michezo, kwa kuzingatia vigezo vilivyobainishwa na Ofisi ya Msajili
wa Hazina na kwa kufuata taratibu zingine za kufanya uteuzi, nimewateua
wafuatao kuwa wajumbe wa Bodi ya TBC;
(i) Bw. William Steven Kallaghe; Mtaalamu wa Uchumi. (M.A – Economics; Head of Public Policy: NBC Bank Tanzania ).
(ii)Bw.
Mustapha Kambona Ismail; Mtaalamu wa Sheria. (LLB - UDSM; Associate
Director, Litigation & Investment – Bank of Tanzania; Advocate of
the High Court of Tanzania).
(iii) Bi. Elimbora Abia Muro; Mtaalamu wa Uhasibu. (CPA, MBA: Senior Internal Auditor, Tanzania Investment Centre).
(iv)
Bw. Mick Lutechura Kiliba; Mtaalamu wa Rasilimali watu. (MBA – Public
Service Mgt; Director of Management: President’s Office – Public Service
Management).
(v)
Dkt. Ayub Rioba; Mtaalamu wa Sekta ya Utangazaji na Utangazaji. (PhD –
Mass Communication; Associate Dean: School of Journalism, University of
Dar Es Salaam) na
6.
Bw. Assah Andrew Mwambene; Mtaalamu wa Sekta ya Habari. ( MSc – Media
Research and Analysis; Director of Information: Ministry of Information,
Culture, Arts and Sports).
Uteuzi wa wajumbe hawa ni kuanzia tarehe 19/02/2016 kwa muda wa miaka mitatu.
3.
Nimalizie kwa kuwapongeza tena wote waliopata uteuzi huu. Tuna
matumaini makubwa toka kwao kwa ajili ya kuboresha ufanisi wa TBC katika
tasnia ya Utangazaji katika ulimwengu wa Teknolojia inayobadilika kwa
kasi kubwa duniani.
Ni
imani yangu kwamba Bodi hii mpya italeta msukumo mpya katika utendaji
wa Shirika ili hata watumishi wanaofanya kazi katika shirika hili
waendelee kujivunia kuwa ndani ya TBC lakini pia Umma wa Watanzania
wajivunie viwango vya utendaji wa Shirika hili.
0 comments:
Post a Comment