Waziri
wa Ujenzi wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Makame Mbarawa ameagiza
Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini TCRA, kusitisha
mara moja mkataba wa Mkurugenzi wa Idara ya Sheria wa mamlaka hiyo,
Elizabeth Nzagi, kwa kushindwa kusimamia ufungwaji wa kifaa cha
kufuatilia mapato ya simu ya ndani katika mitambo ya kuchunguza mapato
katika mitandao ya simu (TTMS).
Waziri
Mbarawa amesema kutokufungwa kwa kifaa hicho kumeisababishia serikali
hasara ya shilingi bilioni 400/= hivyo ameiagiza pia bodi hiyo ya TCRA
kuwasimamisha kazi mara moja, Kaimu Mkurugenzi anayesimamia mfumo wa
uhakiki na usimamiaji huduma za mawasiliano, mhandisi Sunday Richard na
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Sheria, Modestus Ndunguru ili kupisha
uchugnuzi dhidi ya uhusika wao katika kusababisha kifaa hicho
kutokufungwa.
Aidha,
Waziri Mbarawa ametoa onyo kali kwa Mkurugenzi Mkuu wa TRCA, Ally Simba
kwa kutokuwa makini katika utendaji huo huku akimwagiza kuhakikisha
kuwa kifaa hicho kinafungwa ndani ya siku saba.
Profesa
Mbarawa pia ametengua uteuzi wa Mtendaji mkuu wa Wakala wa
Umeme na Ufundi Tanzania (Temesa),Mhandisi Marcellin Magesa kwa
kushindwa kusimamia matengenezo ya magari ya serikali, mitambo
na vivuko.
Kadhalika,
ametengua uteuzi wa Mkurugenzi wa matengenezo ya magari ya
serikali,Prisca Mukama na Meneja wa Karakana ya magari ya
Serikali John Mushina ambao watapangiwa majukumu mengine.
0 comments:
Post a Comment