>>>>>VIDEO <<<<
Katibu
Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania Prof Yunus Mgaya akizungumza na
waandishi wa habari (hawapo pichani) Kuhusu uamuzi wa Tume kufuta
usajili wa vyuo vikuu vishiriki vya Mtakatifu Joseph tawi la Songea.
Picha na Raymond Mushumbusi MAELEZO
……………………………………………………………………………………..
Na Nyakongo Manyama MAELEZO
Tume
ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) imeamua kufuta kibali kilichoanzisha vyuo
vikuu viwili vishiriki vya Mtakatifu Joseph ambavyo ni Chuo Kikuu
kishiriki cha Sayansi ya Kilimo na Teknolojia (SJUCAST) na Chuo Kikuu
kishiriki cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (SJUIT) vilivyopo
Songea.
Akizungumza na waandishi wa habari leo katika ofisi za Tume hiyo, Katibu Mtendaji wa Tume
ya Vyuo Vikuu Tanzania Prof Yunus Mgaya amesema kutokana na mapungufu
yaliyobainishwa na Tume ambayo ni matatizo ya ubora wa elimu na
ukiukwaji wa Sheria za uendeshaji wa Chuo Kikuu kama ulivyobainishwa na
Sheria ya Vyuo Vikuu hii imepelekea Tume kuchukua hatua ya kufuta
usajili wa vyuo hivyo.
“
kutokana na yaliyobainishwa hapo awali tunapenda kutaarifu umma kwamba
,Tume imejiridhisha kuwa hivi vyuo vikuu vishiriki viwili havitoi elimu
ya Chuo kikuu ya viwango stahiki na ukizingatia wanafunzi katika Vyuo
hivi ndio waathirika wakubwa wa matatizo yaliyopo”Alisema Prof Mgaya.
“Napenda
kufafanua kwamba Vyuo vikuu vishiriki tuliyovifutia usajili ni tawi la
Songea na Vyuo vingine vishiriki vya Mtakatifu Joseph vilivyopo Dar es
Salaam na Arusha vitaendelea kufanya kazi kama kawaida”Alisema Prof
Mgaya.
Prof
Yunus Mgaya amesema wanafunzi wote wanaosoma katika vyuo vishiriki
vilivyofutwa usajili wanaarifiwa kuwa watahamishiwa kwenye vyuo vikuu
vingine vinavyofundisha programu za masomo zinazofanana na masomo
wanayosoma hivi sasa chini ya utaratibu uliopangwa.
Amevitaja
vyuo ambavyo watapelekwa wanafunzi walipo katika vyuo vishiriki
vilivyofutwa usajili kuwa ni Chuo Kikuu cha kilimo Sokoine (SUA), Chuo
Kikuu cha Dodoma (UDOM),Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Mwenge(MWECAU) na
Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Ruaha(RUCU).
Amesisitiza
kuwa orodha ya majina ya wanafunzi na vyuo watavyohamishiwa yatawekwa
kwenye tovuti ya Tume hivi karibuni na wale wote wanaonufaika na Mikopo
toka Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu, mikopo yao
itahamishiwa katika vyuo watakavyokuwa wamehamishiwa.
0 comments:
Post a Comment