SIMBA WATUA TAIFA, WACHEZAJI WAKE WAKIKWEPA CHUMBA CHA YANGA, WAINGIA CHUMBA CHA WAANDISHI WA HABARI
Vikosi vyote vya Yanga na Simba, tayari vimewasili kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam tayari kwa mechi yao ya leo.
Lakini
wachezaji wa Simba, ambao walitua uwanjani ahapo baada ya Yanga.
Hawajaingia kwenye chumba cha kubadilishia nguo ambacho kawaida hutumiwa
na Yanga.
Badala
yake wameingia kwenye chumba ambacho hutumiwa na waandishi wa habari
wakati wa mikutano yao kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Wachezaji
wa Simba waliingia kwenye chumba cha waandishi wa habari na mara moja
kuanza maandalizi kwa ajili ya mechi hiyo ambayo itaanza hivi punde.
Hivi karibuni, TFF ilitoa adhabu kwa timu zilizotumia vyumba vya waandishi wa habari au kugoma kuingia vyumbani.
0 comments:
Post a Comment