Wakati
Rais Dk. John Magufuli akitarajia kutangaza safu ya wakuu wa mikoa na
wilaya wapya, imebainika wapo zaidi ya 20 ambao watatemwa kutokana na
sababu mbalimbali za utendaji.
Habari
za kuaminika zinasema miongoni mwa wakuu wa mikoa watakaoachwa wamo
walioshindwa kutatua kero sugu zikiwamo za mapigano ya wakulima na
migogoro ya ardhi ambayo kila kukicha imesababisha watu kadhaa kufariki
dunia.
Kwa
mujibu wa taarifa hizo, pia wamo wakuu wa mikoa ambao wanaweza kuachwa
kutokana na kuwa na umri mkubwa na wanaonyesha wazi hawawezi kwendana
na kasi ya utendaji kazi wa serikali ya awamu ya tano ambayo inatumia
falsafa ya Hapa Kazi Tu.
Habari
hizo zinasema wapo wakuu wa mikoa ambao wameshindwa kutatua migogoro ya
ardhi katika maeneo yao kwa zaidi ya miaka 10 hadi 15 na kusababisha
vurugu kuibuka kila wakati.Miongoni mwa mikoa iliyokithiri kwa migogoro
hiyo ni Morogoro, Tanga na Manyara.
“Wapo
wakuu wa mikoa ambao hawatarudi kutokana na rekodi za matukio, wapo
ambao kwenye maeneo yao migogoro imedumu kwa zaidi ya miaka 10 na
kuendelea, sasa viongozi wa aina hii unadhani watabaki kweli kwenye
Serikali?
“Nakuhakikisha
kule ambako kuna migogoro ya ardhi na mapigano ya kila siku wako
hatarini kupoteza kibarua… unajua mheshimiwa kila siku anajiuliza hivi
inakuwaje mkoa ambao una kamati za ulinzi na usalama za wilaya
zinashindwa kuchukua hatua za kumaliza mapigano haya?
“Inawezekana zinafanya kazi kwa kutegeana au wengine wanakula kwa wafugaji na wakulima.
“Mpaka
wiki iliyopita tumedokezwa kwamba ma-RC 20 hawatarudi katika nafasi
zao kwa sababu wameshindwa kuonyesha kama wanaweza kuwajibika ipasavyo,” kilisema chanzo cha habari hii.
Chanzo
hicho kilisema pia kuwa wengine ambao wako hatarini kutemwa ni wale
wenye umri mkubwa ambao kwa namna moja au nyingine wanapaswa kustaafu.
“Sikutajii
ni mikoa gani kwa sababu hawa wanajulikana vizuri…pale kanda ya ziwa,
nyanda za juu kusini na mikoa ya kaskazini ni maeneo ambayo yataguswa
mno.
“Unajua
Dk. Magufuli na timu yake wanaangalia kwa kina mno hata mikoa ya kanda
ya magharibi nao hawako salama kwa sababu wapo wazee wetu ambao
inaonekana wazi umefika wakati wa kupisha kizazi kingine ambacho
kitasaidia kusukuma mbele gurudumu la maendeleo,”kilisema chanzo chetu.
Kuhusu
wakuu wa wilaya, chanzo hicho kilisema hakuna tofauti na wakuu wa mikoa
kwa vile kila mmoja atapimwa kutokana na namna alivyoweza kusimamia
majukumu ya Serikali tangu alipoteuliwa.
“Jambo
moja kubwa ndugu yangu, hapa kila mmoja atapimwa kutokana na uwezo
wake… nadhani unakumbua Rais mwenyewe alisema anawachunguza, tutarajie
mabadiliko makubwa,” kilisema chanzo chetu.
Hivi
karibu Rais Magufuli, alisema wakuu wa mikoa na wilaya wajiandae
kuwajibika endapo maeneo wanayoongoza yatakuwa na ukosefu wa chakula na
kusababisha wananchi kukumbwa na njaa wakati maeneo mengi ya nchi
yamepata mvua ya kutosha.
Mikoa ambayo imekuwa ikikumbwa na njaa mara kwa mara ni pamoja na Mara, Iringa, Dodoma,Tanga na Shinyanga.
0 comments:
Post a Comment