Kufuatia kutofanya vizuri kitaifa katika mtihani wa kidato cha nne,
shule ya sekondari ya watoto wenye vipaji maalumu, IIboru itaanza
kuwachuja wanafunzi wasio na uwezo wanaopangiwa kusoma shuleni hapo.
Mkuu
wa shule hiyo, Julius Shula amesema licha ya Ilboru kuwa ya kwanza kwa
shule za Serikali nchini, lakini imebaini upungufu katika upatikanaji
wanafunzi.
Amesema kuna wanafunzi kutoka shule za binafsi
wanaopangiwa IIboru, wamebainika hawana uwezo, hivyo kutilia shaka alama
walizopata katika mitihani yao ya kuhitimu darasa la saba.
“Tayari
tumewapa mitihani waliongia kidato cha kwanza, huwezi amini kuna
wanafunzi wanapata alama 0, lakini ukifuatilia matokeo ya kuja hapa wana
wastani wa alama zaidi ya 200 sasa hili ni tatizo kubwa,” alisema.
0 comments:
Post a Comment